title : TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA
kiungo : TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA
TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA
Timu ya kitaifa ya kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji imefanya ziara wilayani Mkuranga ,lengo ikiwa ni kutatua migogoro ya aina zote za ardhi na kuiainisha.
Akizungumza wakati wa ziara wilayani Mkuranga mkoa wa pwani,kiongozi wa timu ya serikali ya ufuatiliaji wa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi Dkt.Martin Ruheta amesema timu hiyo sio ya kisiasa bali ni ya kitendaji na matarajio yao mpaka ifikapo 2020 itakuwa imepatiwa suluhu kama sio kwisha kabisa.
Aidha Dkt.Ruheta amewaahidi wanachi hao kuwa watahakikisha migogoro yao inapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa sababu tume yao ipo makini.
Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Mkuranga Omary kisatu amewaomba wanachi hao kuwa na imani na tume hiyo."wakulima na wafugaji naomba muendelee kudumisha amani na utulivu iliyopo,tume hii ni ya kitaifa ya kuhakikisha haki ya mkulima na mfugaji inapatikana ."alisema Kisatu
Hata hivyo tume hiyo inaundwa na watu mbalimbali akiwemo Ofisa kutoka ofisi ya Rais,Wizara ya Ardhi,Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Ofisa wa ardhi na wa maliasili,lengo kuu ni kuhakikisha migogoro ya ardhi inakwisha nchini
Kiongozi wa Timu ya Serikali ya ufuatiliaji na Utatuzi wa Migogoro na watumiaji wengine wa Ardhi Dkt.Martin Ruheta akizungumza na wakulima pamoja na wafugjia wa kata ya Bupu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Kiongozi wa timu ya Serikali ya ufuatiliaji,Utatuzi wa Migogoro ya watumiaji wa Ardhi, Dkt.Martin Ruhete(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Omary Kisatu.
Katibu Mkuu wa Chama cha wafugaji Tanzania, Magembe Makoye akiwasihi wafugaji wa kijiji cha Matanzi kata ya Beta wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, kutulia na kusubiri taratibu za serikali.
Hivyo makala TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA
yaani makala yote TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/timuya-usuluhishi-wa-migogoro-ya.html
0 Response to "TIMUYA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YATUA MKURANGA"
Post a Comment