title : SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA,
kiungo : SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA,
SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA,
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi Klabu ya Simba, imeshusha majembe mawili ya maana huku lingine likitarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa.
Wakali hao wamekuja kufanya majaribio ili waweze kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni beki wa kati, Mghana Moro Lamine na straika Mtogo Hunlede Kissimbo Ayi walianza kufanya mazoezi na Simba juzi Jumatatu jioni katika Uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam chini ya uangalizi wa Kocha Patrick Aussems ambaye ndiye atakayetoa kauli ya mwisho juu ya usajili wao wapewe mikataba au wafyekelewe mbali.
Si hao tu, mabosi wa Simba katika kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao zaidi, straika mwingine kutoka nchini Namibia anatarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya majaribio kama hayo.
"Hawa wachezaji tumewaleta kwa ajili ya majaribio na si hawa wawili tu bali watakuwa watatu na mwingine straika kutoka Namibia mtamuona siku si nyingi atawasili nchini," alisema mmoja wa kigogo wa Simba ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.
"Tutawatumia wachezaji hawa katika mashindano ya SportPesa na itakuwa kama sehemu yao ya majaribio ili kuona kama wanauwezo wa kuisaidia Simba ili tuwasajili na kama watakuwa hawana uwezo kwa mujibu wa kocha wetu tutaachana nao," alisema.
Hivyo makala SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA,
yaani makala yote SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA, mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/simba-washusha-vifaa-vipya-kutoka-ghana.html

0 Response to "SIMBA WASHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA GHANA,"
Post a Comment