SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON

SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON
kiungo : SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON

soma pia


SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON

Muandaaji wa michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo.
Muandaaji wa michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ili kuzindua michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizindua mashindano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akionyesha medali ya shaba baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa kilomita tano katika michuano ya Mirerani Tanzanite Marathon. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiongoza mbio za kilomita tano katika michuano ya riadha ya Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakishuhudia mbio za Mirerani Tanzanite Marathon zikitaka kuanza. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiwa na baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Mirerani Tanzanite Marathon yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 

…………………………….

MWANARIADHA mwanajeshi wa JWTZ Faraja Damas ameng’ara kwenye mbio za Mirerani Tanzanite Marathon kilomita 21 zilizozinduliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:14.

Katika mbio hizo zilizofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Michael Joseph alishika nafasi ya pili kwa kutumia saa 1:34.

Mshindi wa tatu alikuwa Stephano Huche aliyetumia muda wa saa 1:34 huku Failuna Mtanga akishika nafasi ya kwanza kwa wanawake katika kilomita 21 kwa kutumia saa 1:09. 

Angelina Daniel alishika nafasi ya pili kwa wanawake kilomita 21 kwa saa 1:14 na nafasi ya tatu ni Rosalina Fabian kwa saa 1:16 na mbio za watoto kilomita tano wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Blue Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani, Sarah Barakael, Clara Flavian na Shangwe Isack, walingara kwa kuongoza michuano hiyo. 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizungumza wakati akizindua mbio hizo aliwataka maofisa michezo wa mikoa na wilaya kufuatilia vipaji vya michezo mashuleni na kutokaa maofisini. 

Shonza alisema vipaji vingi vipo kwenye ngazi za shule hivyo maofisa michezo wa wilaya na mikoa wafuatilie hilo kwa manufaa ya sekta ya michezo nchini. 

Alisema ana wapongeza waandaaji wa mashindano hayo ambayo japokuwa ni mara ya kwanza lakini wamejitahidi kuepuka changamoto mbalimbali ambazo huwa zinajitokeza kwenye michezo mbalimbali. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alisema mashindano hayo yametumika kuweka historia ya mashindano makubwa ya riadha kufanyika kwenye eneo la mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 

Mhandisi Chaula alisema katika wilaya hiyo hakujawahi kufanyika mashindano ya riadha ila kupitia Mirerani Tanzanite Marathon jina la Simanjiro linaingia kwenye historia ya kufanyika mashindano makubwa. 

Katibu wa shirikisho la riadha Tanzania, Wilhelim Gidabuday alisema baadhi ya wakenya walizuiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kukosa vibali. Gidabuday alisema hawana nia mbaya ya kuwazuia wakimbiaji hao wanne wa Kenya ila kutokana na kutokuwa na vibali hivyo hawakuruhusiwa kushiriki. 

Muandaji wa mashindano hayo ya Tanzanite Mirerani Marathon, Charles Mligo (Mnyalu) alisema lengo la mashindano hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli kwa kutangaza utalii wa madini ya Tanzanite. 

Mnyalu alisema baada ya Rais Magufuli kuagiza ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite kujengwa nao wakaamua kuanzisha mashindano hayo ili kutangaza madini ya Tanzanite ambayo hapa duniani yanapatikana mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara pekee


Hivyo makala SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON

yaani makala yote SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/shonza-azindua-mirerani-tanzanite.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SHONZA AZINDUA MIRERANI TANZANITE MARATHON"

Post a Comment