title : Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote
kiungo : Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote
Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote
Meneja Masoko Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dar es Salaam, Evord Mwauzi amesema tatizo la uandishi wa barua kwa wanafunzi ikiwamo wa elimu ya juu bado ni tatizo kubwa. Meneja huyo,ameyasema hayo leo Januari 18.2019 wakati wa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Afrika yaliyofanyika katika ofisi za Posta zilizopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala.
Amesema, katika utekelezaji wao wa majukumu, wamebaini kuwa uandishi wa barua hasa kwa wanafunzi wakiwamo wa vyuo vikuu bado ni tatizo kubwa hapa nchini. Akiwaelezea wanafunzi hao jinsi shirika hilo la posta linavyotoa huduma,Mwauzi ametoa wito kuwa siku zijazo baadhi ya huduma za Shirika la Posta ziingizwe katika mitaala ya elimu.
Amebainisha kuwa, Shirika la Posta limetenga siku ya Jumatano kwa ajili ya kutoa elimu hasa ya uandishi wa barua kwa wanafunzi na huduma wanazozitoa na kuzitaka shule kuwatumia maombi iwapo wanahitaji elimu hiyo. Ameongeza, hali hiyo inatokana na kuwa namabadiliko ya teknolojia, kitu ambacho kimepelekea pia hata hali ya watu kumiliki masanduku ya posta kupungua….., lakini utaratibu uliopo mtu yoyote anayekuja nchini kuwekeza lazima awe na sanduku la Posta.
Hata hivyo alibainisha kwa kwa sasa Shirika la Posta linatoa kila huduma kwa kutumia njia ya mtandao ikiwamo huduma ya Post Code ambayo humfanya mtu, kufahamu nyumba ya mtu anayoitafuta iko mahali gani ikiwa tu atakuwa akifahamu jina la mtaa na barabara husika.
Kwa upande wake, Afisa Masoko Mwandamizi wa shirika hilo, James Musyangi amesema maadhimisho hayo ya Siku ya Umoja wa Posta Afrika yalianzishwa Januari 17, mwaka 1980 yakiwa na lengo la kuhakikisha uelewa wa wafanyakazi wa Posta Afrika kuwa mmoja katika mambo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao na kutetea maslahi na hata katika nyanja ya elimu pia.
Aidha,Afisa Masoko huyo Mwandamizi aliwatembeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala katika vitengo mbalimbali vya shirika hilo ikiwamo maeneo ya kutuma barua za ndani na nje ya nchi na ukaguzi wa mizigo inayotumwa kutoka ndani kwenda nje ya nchi na inayotoka nje ya nchi kuingia nchini kama ni halali na inastahili kulipiwa kodi ama la.
Hivyo makala Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote
yaani makala yote Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/sheila-la-posta-lahamasisha.html
0 Response to "Sheila la posta lahamasisha ufundishwaji wa uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote"
Post a Comment