SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA
kiungo : SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

soma pia


SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Na Nyamagory Omary wa PMO
Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House). 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo  Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro. 
Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Agriculture  Group Ltd, na SUGECO. 
Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni  kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo  kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (greenhouse). 
“Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”alisisitiza Mavunde. 
Aidha, Amewataka vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua na changamoto za ajira na kuelezea umuhimu wa kilimo katika kuongeza pato la Taifa na kuchangia katika uchumi wa viwanda nchini.

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na mtaalamu wa masuala ya kilimo cha kisasa kwa  kutumia mabwawa ya samaki (Acquculte) alipotembelea kukagua mradi huo, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Ofisi hiyo Mhe Stella Ikupa
 Manaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia kiazilishe katika moja ya banda la maonesho la vijana walioshiriki mafunzo ya Kilimo cha kisasa cha kitalu nyumba. Katikati ni Mhe.Stella Ikupa anayeshughulikia Wenye Ulemavu na Kushoto ni Mhe.Anthony Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira).

 Baadhi ya viongoizi wakishuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (Wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Muongozo wa masuala ya kilimo cha Kitalu Nyumba wakati wa warsha hiyo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akikagua biskuti zilizotengenezwa kwa kutumia nanasi ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotengenezwa na vijana waliopewa mafunzo na SUGECO wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario .
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akiangalia mapapai yaliyolimwa kwa njia ya kisasa katika mashamba ya SUGECO katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro.


Hivyo makala SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

yaani makala yote SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/serikali-yazipa-kandarasi-ya-thamani-ya_6.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA"

Post a Comment