SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO
kiungo : SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

soma pia


SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

SERIKALI inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji. 

Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo.

Profesa Mkumbo alifanya ziara katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kujionea utendaji wa kazi zao na zaidi kuona changamoto zinazowakabili watumishi hao na mamlaka husika na namna ya kuzitafutia ufumbuzi. Profesa Mkumbo alisema katika fedha hizo zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.

Alisema katika Miji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na Handeni BILIONI 112.5(HTM). “Matarajio ya Serikali ni kuhakikisha inapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji vijijini na mijini na kufikia malengo yaliyojiwekea hadi kufikia mwaka huo wa 2025”Alisema Profesa Mkumbo.

Aidha lisema mchakato wa miradi hiyo mikakati umekwisha anza kwa hatua za awali ya usanifu na kupata Mtaalamu mshauri kwa ajili ya miradi hiyo katika Miji ambayo imebainishwa kunufaika na fedha hizo kwa nchi nzima. Alisema hadi kufikia juni mwaka huu miradi hiyo itakuwa imekwisha dizainiwa na mwezi Sept wakandarasi watatkiwa kuwa katika maeneo ya kazi katika miji hiyo 28 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka makandarasi kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na watambue Serikali haitomzulumu mkandarasi yoyote na fedha zao zitalipwa bila ya mashaka yoyote. “Tunajua madai ya makandarasi wengi nchi nzima lakini tutawalipa waondoe shaka koila mwezi tulipa shilingi Bilioni 8-12 hivyo tutwalipa tu”Alisema.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema changamoto kubwa kwa sasa mkoani hapa ni namna ya kuongeza huduma ya taka ndani ya Jiji.“Mbali na fedha zilizoainishwa na Katibu Mkuu lakini tunatarajia kupokea zaidi ya shilingi bilioni 400 kwa ajili ya miradi ya maji taka,kubadilisha miundombinu ya mabomba,ujenzi wa matank”Alisema Mhandisi Hilly. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kulia akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly


Hivyo makala SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

yaani makala yote SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/serikali-kutumia-shtrilioni-13-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO"

Post a Comment