title : SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA
kiungo : SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA
SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA
Serikali kuendesha operesheni kubwa kuwaondoa wavamizi wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na watu wengine wanaofanya shughuli zisizo halali katika misitu na mapori yaliyohifadhiwa kisheria zikiwemo hifadhi za misitu ya serikali Kuu na halmashauri za vijiji.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo wakati akisoma maazimio ya kikao cha mawaziri watano kilichofanyika mkoani Kigoma leo kutafuta utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi na Mapori ya Akiba ya Moyowosi.
Jafo alisema, wale wote waliovamia hifadhi wanatakiwa kuondoka kwa hiari kabla ya zoezi la kuwaondoa kwa lazima, operesheni hiyo itafanyika wakati wowote ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 2019.
Na kusisitiza kuwa wale wenye mazao katika hifadhi na mapori ya akiba wanaweza kuomba idhini ya kuvuna mazao yao.Jafo alisema Serikali imetenga jjmla ya hekta 10,012.61 kutoka kwenye hifadhi ya msitu wa Makere kusini kwa ajili ya kilimo na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu ambapo Hekta 2,174 kwa ajili ya kijiji cha Mvinza, hekta 2,496 kwa kijiji cha Kagerankanda na halmashauri ya wilaya ya Kasulu Jumla ya hekta 5,342.61.
Kwa mujibu wa Jafo uamuzi huo unafuatia kuwepo kwa changamoto katika maeneo ya hifadhi za misitu na mapori ya Akiba ambapo maeneo mengi yamevamiwa kwa shughuli za kilimo na ufugaji na hivyo kupoteza uoto wa asili katika hifadhi na mapori ya Akiba.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakiwasikiliza Mawaziri walipofanya ziara katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere lililopo Kasulu Kigoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakati wa ziara ya Mawaziri watano kukagua eneo la hifadhi la Msitu wa Makere.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akikatiza katika moja ya vichaka vilivyopo kwenye hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma wakazi wa ziara ya Mawaziri watano kukagua msitu.
Mawaziri Dk Hamis Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii, Suleiman Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwasikiliza wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili alipofanya ziara katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo akiwaongoza Mawaziri wenzake kukagua maeneo mbalimbali katika hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
Moja ya eneo ndani ya hifadhi ya Msitu wa Makere uliopo Kasulu Kigoma ambapo Mawaziri watano walibaini uendeshaji shughuli za kilimo ukifanyika ndani ya hifadhi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima (kushoto), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika gari wakati wa kukagua hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
Hivyo makala SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA
yaani makala yote SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/serikali-kuendesha-oparesheni-kubwa.html
0 Response to "SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA"
Post a Comment