title : PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA
kiungo : PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA
PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Uchumi wa Viwanda inayohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, akina mama na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali jijini Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kuwatembelea watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko huo na kuhimiza uwajibikaji, ambapo alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, makundi yaliyopatiwa mikopo ambayo ni kundi maalumu la walemavu la Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kutekeleza sera ya Uchumi wa viwanda kwa vitendo kwani wanazalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni mvinyo, viungo vya mchuzi, viungo vya chai, siagi ya karanga, mango pickle na mabeji ya wanafunzi wa shule za awali, za msingi na vyuo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM wakati wa ziara ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA
yaani makala yote PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ptf-yapongezwa-kwa-kutekeleza-sera-ya.html
0 Response to "PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA"
Post a Comment