title : OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.
kiungo : OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.
OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.
Anaandika Dixon Busagaga, Moshi.
OPERESHENI ya kukamata Dawa za kulevya inayoendelea mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kukamata kilogramu 320 na Dawa za kulevya aina ya Mirungi zikiwa kwenye gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za usajili T 308 DMC ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
Hili ni tukio la pili ndani ya siku sita kwa Jeshi la Polisi kufanikiwa kukamata kiasi kikubwa cha Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ambapo tukio la karibuni kikosi cha Pikipiki cha jeshi hilo kilifanikiwa kunasa kilogramu 80 za Mirungi iliyokuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki kutoka nchi jirani ya Kenya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa Dawa hizo za kulevya katika eneo la KIA zikiwa njiani kusafirishwa kuelekea Arusha kutokea nchi jirani ya Kenya .
“Tulipata taarifa uwepo wa gari nyeusi ambayo mwendo wake ulitiliwa shaka na askari wetu ,na kila walipokuta askari ilikuwa ikiwasha taa huku ikiwa mwendo wa kasi,ndipo katika kituo cha KIA askari walizuia magari yote na kufanikiwa kuikamata hiyo gari”alisema Kamanda Issah.
“Wale watu waliokuwa kwenye hii gari baada ya kuona askari wanawafuata walikimbia na kupanda pikipiki zilizokuwa pembeni yake na kutokomea kwa uelekeo wa Arusha na hata hii gari inaonekana uelekeo wake ulikuwa ni huko huko Arusha na tumefanikiwa kuikamata.”aliongeza Kamanda Issah.
Alisema gari lililokuwa limebeba mzigo huo wa dawa zakulevya litakuwa chini ya jeshi la Polisi huku akitoa wito kwa mmiliki wa gari hilo kujitokeza mwenyewe kabla hatua za kufuatilia katika vyombo vingine vya dola kuanza .
Katika tukio la hivi karibuni Polisi walikamata Majani ya Miringi yaliyokuwa yamefungwa katika vifurushi vidogo vidogo zaidi ya 50 na kisha kuwekwa kwenye mfuko mmmoja mkubwa maarufu kama Kiroba huku wahusika wakitumia pikipiki maarufu kama Bodaboda.
Alisema kundi la wasafirishaji wa Dawa hizo za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kutoka nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Holili pindi linapoingia barabarani limeonekana kuwa tishio na hatari kwa usalama wa watu wengine barabarani kwa namna wanavyoendesha pikipiki zao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiwa ameshikilia dawa za kulevya aina ya mitungi baada ya kukamatwa katika eneo la KIA.
Magunia yenye Dawa za kulevya aina ya Mirungi yakipimwa katika mzani mara baada ya kukamatwa yakisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
Gari aina ya Toyota Alphasad lenye namba za s usajili T 308 DMC lilikuwa kumbeba dawa hizo aina ya Mitungi kilogramu 380.
Hivyo makala OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA.
yaani makala yote OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/operesheni-jeshi-la-polisi-kilimanjaro.html
0 Response to "OPERESHENI JESHI LA POLISI KILIMANJARO YAKAMATA KILO 400 YA MIRUNGI NDANI YA SIKU SITA."
Post a Comment