NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020

NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020
kiungo : NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020

soma pia


NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020

NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO.

Baraza maalumu la madiwani pamoja na Baraza la wafanyakazi katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma limepitisha Rasimu ya mpango wa bajeti 2019/2020 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo.

Akisoma rasimu ya bajeti hiyo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo Ofisa mipango wa Halmashauri TeklaNyoni alisema kuwa mapendekezo ya bajeti hiyo imezingatia dira ya Halmashauri ,mwelekeo wa Halmashauri pamoja na miongozo mbalimbali iliyotolewa na serikali na kulenga kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi 2015-2020

Awali Tekla alitoa taarifa kwa waheshimiwa madiwani na kisha kwenye baraza la wafanyakazi kuwa pamoja na mambo mengine mapendekezo ya bajeti hizo zimezingatia vipaumbele vilivyoibuliwa na wananchi kutoka katika vijiji na kisha kuwasilisha vipaumbele hivyo ofisi ya mkurugenzi.

Aliwathibitishia waheshimiwa madiwani pamoja na baraza la wafanyakazi katika vikao tofauti kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imekasimia kuwa na bajeti ya shilingi 24,212,575,600.ambapo kati ya fedha hizo shilingi 1,765,714,100 sawa na asilimia 7 zitatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 18,371,513,00 sawa na asilimia 76kwa ajili ya mishahara na shilingi 2,658,621,500 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo ni sawa na asilimia 11 ya fedha kisiwa na jumla ya shilingi 1,416,727,000 sawa na asilimia 6 kuwa ni makusanyo ya Ndani ya Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Daniel Nyambo aliwataka waheshimiwa madiwani kupitia mapendekezo ya bajeti hizo kwa umakini na kuazingatia mahitaji ya vipaumbele hizo katika maeneo yenye uhitaji badala ya kila diwani kulalamikia kuingizwa vipaumbele vyake kwanza.

Hata hivyo aliwataka madiwani hao kufahamu kwamba fedha hata siku moja haitoshelezi mahitaji na kinachotakiwa katika halmashauri hiyo ni kujipanga ili kukamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika na sio vinginevyo.

Nyambo pia aliwataka madiwani wenzake kuunda kamati ya kupitia pendekezo la chanzo kipya cha mapato kinachopendekezwa cha kuwa na mnada wa ng`ombe katika Halmashauri hiyo ili kujiridhisha kama chanzo hicho cha mapato kinaweza kusaidia Halmashauri hiyo kuinua mapato kulingana na Ng`ombe waliopo na kujihadhari na chanzo hicho kutoa mwanya wa wafugaji kuingiza mifugo yao katika Halmashauri hiyo 

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Evance Nachimbinya aliwaomba waheshimiwa madiwani kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao kuibua miradi ya maendeleo kama kujenga vyoo vya shule zahanati na kuanza kuitekeleza mpaka hatua ya boma na Halmashauri itashughulika vifaa vya viwandani ili kukamilisha miradi hiyo alisema mkurugenzi huyo.

Lakini pia mkurugenzi huyo aliwataka madiwani hao kuhamasisha wananchi wao kuhusu kulima mazao kwa wingi ili wapate chakula cha ziada na biashara ili halmashauri iweze kupata mapato yatakayoiwezesha halmashauri kukamilishia umaliziaji wa miradi ya wananchi wake.

Kikao cha Kupitisha mapendekezo ya bajeti 2019-2020 kilikuwa cha siku moja ambapo kilitanguliwa na baraza la wafanyakazi na kisha baraza la madiwani la Halmashauri hiyo .
Tekla Nyoni akiwasilisha mpango wa bajeti wa Halmashuri hiyo kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Hivyo makala NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020

yaani makala yote NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/namtumbo-wapitisha-rasimu-ya-mpango-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NAMTUMBO WAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2019/2020"

Post a Comment