title : NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO
kiungo : NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO
NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO
Na Munir Shemweta, Biharamulo
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kujipanga na kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza migogoro ya ardhi na wasipotekeleza majukumu yao vizuri atawawajibisha.
Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo katika ofisi za halmashauri hiyo mkoani Kagera, Dk. Mabula alisema pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo lakini watumishi wa sekta hiyo wanapaswa kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kupunguza migogoro ya ardhi na wakati huo kuwawezesha serikali kukusanya mapato kupitia sekta ya ardhi.
"Kama kazi haziendi migogoro ya ardhi haiwezi kuisha na ninyi hapa mna viwanja vichache lakini mmeshindwa kuviingiza katika mfumo hivyo mkimaliza kuviingiza viwanja hivyo hapo mnaweza kurekebisha takwimu" alisema Dk Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaziangalia idara za ardhi katika halmashauri zao kwa kuwa hakuna miradi inayokamilika bila kuhusisha ardhi hivyo sekta hiyo ni muhimu na inapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akikagua jalada la ardhi katika ofisi ya masijala ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Sospiter Mwishamba na kushoto ni Mpimaji Ardhi Vedastus Masige
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Novatus Babu alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasili Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera alipofanya ziara ya kushtukiza katika halamashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO
yaani makala yote NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-mabula-awaonya-watendaji.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO"
Post a Comment