title : MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE
kiungo : MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE
MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kusini Merndrad Kigola kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ameitaka Serikali kueleza ni hatua gani inazochukua ili
kukomesha mauaji ya watoto katika Mkoa wa Njombe.
Akiuliza swali hilo leo Januari 30, 2019 bungeni Mjijini Dodoma, Kigola ameuliza ni mkakati gani uliopo katika kukomesha mauaji hayo ambayo yamesababisha hofu kubwa kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akijibu swali hilo , Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema kuna hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kukomesha mauaji hayo na tayari tangu Januari 28 mwaka huu Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako amekutana na kamati za ulinzi na usalama ya mkoa wakiendelea na vikao vya ndani.
"Tunaamini wote wanaojihusisha na vitendo hivyo watapatikana na sheria
itachukua mkondo wake. Tunayo orodha ya maji ya watu ambao wanahusika na matukio hayo na sababu za kufanya hivyo ni mambo ya imani za kishirikiana,"amesema Lugola huku akisisitiza wanaofanya matukio hayo ya mauaji hayo waache mara moja.
Kwa kukumbusha tu wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua dhidi ya kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo, idadi ya watoto waliouliwa
imefikia 13 kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa.
Wakati huohuo Lugola amezungumzia hatua ambazo Serikali inazichukua ili
kupunguza msongamano wa mahabusu katika magereza nchini.Amesema hayo leo wakati anajibu swali aliloulizwa kuhusu hatua ambazo Serikali inachukua katika gereza la Mlele ambalo idadi ya mahubusu imekuwa kubwa.
"Kuna hatua ambazo Serikali inachukua maeneo yote ya magereza ambayo yanayonekana kuzidiwa na idadi ya mahabusu.Kwa gereza la Mlele naomba nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa hatua ambazo anazochukua za kufanikisha ujenzi wa gereza la Mlele,"ameseme Lu
gola.
Hivyo makala MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE
yaani makala yote MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mbunge-ataka-kufahamu-hatua.html
0 Response to "MBUNGE ATAKA KUFAHAMU HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUKOMESHA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE"
Post a Comment