title : MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE
kiungo : MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE
MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
AMEWACHANA!Ndivyo unavyoweza kuelezea kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kuamua kuwachana ‘Live’ baadhi ya wasanii ambao wanamdharau na kumkejeli Steve Nyerere.
Akizungumza leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Makonda amesema wasanii ni vema wakajenga tabia ya kuheshimiana.”Nimeamua kukutana na wasanii na nikamuomba Steve Nyerere anisaidie kuwaambia lakini baadhi yenu mnasema Steve ndio nani.
“Mbona mnapokua na matatizo yenu au mnapopatwa na misiba mnamwambia Steve Nyerere aje kwangu aniambie.Tuheshimiane hata kama tulisoka wote lakini hatufanani , hivyo lazima tujenge kuheshimiana,”amesema Makonda.
Makonda hakusita kuwaambia wasanii hao kuwa kuna baadhi yoa hata wanapokamatwa wanaomba msaada wa Steve Nyrere afikishe ujumbe kwake na leo hii anamuomba amsaidie kuwaambia anataka kukutana na wasanii wanamkejeli.
Makonda amesema kwake yeye hana msanii mkubwa wala mdogo na hivyo ataamua tu amtumie msanii gani kwenye jambo la aina gani. “Kwangu wasanii wote mnayo nafasi sawa, asitokee mmoja wenu akajiona kwanu anayo nafasi kubwa kuliko mwingine.Ndio maana nasema kila mmoja amheshimu mwenzake na kujenga utamaduni wa kupenda ili mambo yaende,”amesema Makonda.
Ametumia nafasi hiyo kuwahamiza wasanii kuwa wamoja kwani kinyume na hapo hakuna ambacho watafanikiwa.”Naomba muwe wa moja na nitafurahi mkiwa wamoja na kujadili mambo yenu. Acheni majungu.” Pamoja na mambo mengine Makonda ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati mbalimbali ambayo ameipanga kwa ajili ya kuwainua wasanii huku akiwataka kuangalia namna ya kutatua changamoto ambazo zinawakabili wasanii.
Pia Makonda amewataka wasanii wa fani zote kujitathimini na kutambua thamani yao ili kuondoa malalamiko yaliyopo kabla na maada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali nchini.
Pia amesema ni wakati sahihi wa kuangalia suala la bima ya afya kwa wasanii na kutumia nafasi hiyo kuwaleza lengo la kukutana nao ni kutaka kuwasikiliza zaidi wao ili kuwa na ukurasa mpya wa wasanii wa tasnia zote.
Hivyo makala MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE
yaani makala yote MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/makonda-awachana-live-wasanii-kisa_31.html
0 Response to "MAKONDA AWACHANA ‘LIVE’ WASANII KISA... STEVE NYERERE"
Post a Comment