LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO
kiungo : LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

soma pia


LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

Na. Vero Ignatus, Arusha


Waumini wa dini ya Kikristo Jijini Arusha wametakiwa kulipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa siyo kuiba, kwani wao wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii inayowazunguka

Hayo yamesemwa na Makamu wa Askofu Dayosisi ya kaskazini Kati Gidion Kivuyo alipokuwa akihubiri katika katika la KKKT Usharika wa Engarenarok uliopo Jiji Arusha.

Amesisitiza kuwa kumjua Mungu Pamoja na kukataa rushwa, kutokuiba mali ya serikali kwani hata neno la Mungu linasisitiza kulipa kodi.'' Lipeni kodi ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu nanukuu maandiko siyo mimi''Alisema Mchungaji Kivuyo.Amewataka waumini hao kuishi maisha safi ya kuigwa maana ni chachu katikati ya kwa watu wengine wanaowatazama ambapo uadilifu, nidhamu na uchaji ambao kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwao.

Amewasisitiza kuwa na utayari na kujifunza,akisema uanafunzi ni pamoja na kujikana wenyewe, kuepuke mambo ambayo siyo sahihi katika imani yao, na waenende sambamba na neno la Mungu linavyowataka.

Amewataka kujifunza na kutafakari siyo kufuata mkumbo bila Kuwa na mipangilio katika maisha bila kusahau uzalendo na kuchunguza mambo kwa kina.
'' Kuna watu wanaojifunza bila kufuzu mafunzo ya kweli, msiwe watu wasiopenda mema na kupenda anasa bali dumuni katika kweli ya Mungu ambayo itawaweka huru,epukeni kutangishwatangishwa kwenye mafundisho ya uongo nakupenda fedha" Alisema.

Amewataka kuwa na uelewa kwamba Imani haijengwi juu juu bali kwa mafundisho, huku akiwataka kuepuka utumwa ambao utawafanya mateka.
Amewaonya waumini hao na kuwataka makini na mafundisho ya uongo ambayo yanayogusa hisia lakini hayafundishi ukweli bali ni misisimko na wala hayana ukweli sawasawa na Mungu anavyoamuru.

Kadhalika amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii iliwaweze kupata mafanikio sambamba na kulipa kodi ya serikali, na siyo kuzurura hovyo. '' Wacheni kuzunguka kwenye maombi kila mahali unachelewa wenzio wamefungua biashara zao na wamefanikiwa, wewe kutokana na kutokutulia kwako unabakia ukilaumu'' alisema

Amewaataka viongozi wa kanisa hilo kuwakumbusha waumini wao neno la Mungu mara kwa mara na kuwafundisha, Kutambua, kujuta, kutubia, kupokea, kuishi maisha na dhamiri safi mbele za Mungu. Amewataka kuweka malengo ya mwaka 2019 na siyo kuishi bila utaratibu ili waweze kurejea katika msingi mzuri wa kanisa hilo.


Hivyo makala LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

yaani makala yote LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/lipeni-kodi-ya-serikali-wacheni-kona.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO"

Post a Comment