KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.
kiungo : KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

soma pia


KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

Anaandika Dixon Busagaga,Moshi 

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa Mazingira lijulikanalo kama LEPAJE limezindua kampeni ya uoteshaji wa miti ya matunda juu Makaburi kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya uharibifu wa mazngira nchini kwa kubadili wafu kuwa mti wa matunda.

Katika kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi huu katika kijiji cha Kifuni juu kata ya Kibosho Umbwe wilaya ya Moshi vijijini,mkoani Kilimanjaro,tayari miti ya matunda ya Parachichi imeoteshwa katika makaburi matano ya mfano huku makaburi zaidi ya 200 yakitaraji kuoteshwa kupitia kampeni hiyo.

Leonard Massawe ni mkurugenzi wa Shirika la Lepaje anasema katika kijiji hicho wamekubaliana kuotesha miti ya matunda ya muda mfupi na yanayopendwa na jamii ambayo yatakuwa tayari kuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Kwenye maeneo yetu haya ya baridi tumeamua kuotesha ,miti ya matunda ambayo yanastawi vizuri na ambayo yanapendwa zaidi na jamii yetu ya huku,tumeotesha Parachichi za kikonyo ,hata hivyo kampeni hii inahitaji kuungwa mkono na Serikali ,Wanahabari,viongozi wa Dini,taasisi za elimu na jamii kwa ujumla”alisema Massawe.

Amesema Makaburi matano ya mfano yaliyooteshwa miti ya matunda ni ya familia yake akiwemo mama yake mzazi na kaka zake wawili akieleza kuwa kampeni hiyo ni rahisi huku akisisitiza jamii kuinga mkono ili kufikia lengo.

“Kuishawisi jamii kuotesha miti ya matunda juu ya kaburi inahitaji ujasiri mkubwa ,mimi nimeotesha mti wa tunda la Parachichi kwenye kaburi la Mama yangu mzazi ili iwe mbegu ya utunzaji wa mazingira Duniani”alisema Masawe.Alisema muda umefika kwa jamii ya Wachaga kubadili mtazamo wa kuotesha majani yajulikanayo kama “Isale” na badala yake waoteshe miti ya matunda muda mfupi tu baada ya kumzika ndugu yao.

Alisema mwaka 2019 ni mwaka wa kubadili wafu kuwa Matunda katika mkoa wa Kilimanjaro huku akiitaka jamiii katika makaburi ya ndugu zao hata kama walizikwa miaka mingi iliyopita na kwamba hali hiyo itachangia kuboresha hali ya hewa kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Mmoja wa wananchi katika kijiji hicho Lucia John amesema uoteshaji wa miti a matunda katika kaburi pia utasaidia kuimarisha afya kwa jamii lakini pia utachangia uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuuza matunda na mengine yanaweza kusafirishwa nje ya nchi.

Hii ni kampeni ya 32 kwa shirika lisilo la kiserikali la kuhifadhi mazingira ambapo awali limefanya kampeni za kuotesha miti katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro kupitia mchezo wa riadha iliyojulikana kama Lepaje Marathon.






Hivyo makala KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

yaani makala yote KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kilimanjaro-wazindua-kampeni-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI."

Post a Comment