title : KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA
kiungo : KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA
KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KESI ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na wenzao saba inayonguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Januari 17, 2019. Mbowe na Matiko watandelea kusota rumande hadi tarehe tajwa kufuatia Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washtakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 26, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana.
Wakili wa upande wa mashtaka Profesa Abdallah Safari amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani. Profesa Safari alihoji kuhusu rufaa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kueleza kuwa shauri limeitwa kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya kueleza hayo, Profesa Safari alimuuliza Wakili Kadushi kama rufaa waliyoikata ilikuwa chini ya hati ya dharura na kama hawakufanya hivyo ni kwa nini...? Katika majibu yake Wakili Kadushi ameeleza kuwa hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17, 2019 huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.
Hivyo makala KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA
yaani makala yote KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kesi-ya-mbowe-na-wenzake-yapigwa.html
0 Response to "KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA"
Post a Comment