title : Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga
kiungo : Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga
Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa la Moyoni kwa kuwaeleza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu pamoja na viongozi wenzake kwamba wamejipanga vyema katika kuwatumikia wananchi wa Kasulu.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo ya kufurahishwa baada ya kutembelea miradi minne ya sekta ya afya pamoja na barabara wilayani humo na kuridhishwa Sana na usimamizi mzuri wa miradi Hiyo. Miradi aliyo ikagua ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Lami katika Halmashauri ya mji wa Kasulu, ukarabati wa Hospitali ya Mji Kasulu na Kituo cha Afya Kiganamo.
Pia katika halmashauri ya wilaya Kasulu Waziri Jafo alifanikiwa kukagua kituo kimoja cha Afya cha Rusesa ambacho ni moja ya kituo cha afya kati ya vituo vya afya vitatu vilivyojengwa na Serikali katika halmashauri hiyo.
Katika Zara hiyo waziri Jafo alimshukuru sana Mhe. Daniel Nsanzugwako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini na Mhe. Vuma Mbunge wa Jimbo la Kasulu vijijini kwa kufikisha kilio cha wananchi wao serikalini hadi serikali imefanikisha kutekeleza miradi hiyo muhimu yenye maslahi mapana kwa wananchi.
Wakati huo huo waziri Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwezesha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa barabara ya Lami Kasulu Mjini kwani mkandarasi anayejenga barabara hiyo iliyo chini ya TARURA amekwama kupata malighafi za CRS ambayo inapatikana kwa eneo la wakandarasi wa Ki-China anayejenga barabara za TANROADS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akipata maelezo toka kwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu kuhusu ujenzi wa barabara ya lamo ya katikati ya mji wa Kasulu
Barabara ya Kasulu inayojengwa kwa kiwango cha Lami
Kituo cha Afya Rusesa kinachoendelea kujengwa katika Wilaya ya Kasulu
Hivyo makala Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga
yaani makala yote Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kasulu-mmejipanga-jafo-alonga.html
0 Response to "Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga"
Post a Comment