title : HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA
kiungo : HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA
HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA
*Ni kauli ya wateja wakubwa mkoani Arusha wanaomiliki viwanda vikubwa
*Wakiri kuimarika kwa umeme imekuwa chachu kwao kuongeza uzalishaji
Na Said Mwishehe,Arusha
*Wakiri kuimarika kwa umeme imekuwa chachu kwao kuongeza uzalishaji
Na Said Mwishehe,Arusha
HATUNA tena za umeme katika Mkoa wa Arusha!Hivyo nidvyo ambavyo wamiliki wa viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali mkoani Arusha wanavyoeleza baada ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), kuboresha upatikanaji wa umeme.
Wakizungumza mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao wamepata nafasi ya kutembelea viwanda vilivyopo mkoani Arusha jana na kupata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wamiliki wa viwanda hivyo wamekiri kwa sasa hali ya umeme inaridhisha kwai huko nyuma hali ilikuwa mbaya na ilisababisha hata uzalishaji wa bidhaa kutofanyika kwa kiwango ambacho walikuwa wanakitarajia.
Wamiliki hao wamesisitiza kuwa kuimarika kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika wameongeza uzalishaji huku wengine wakifafanua wameamua kuanzisha na viwanda vingine kwani hivi sasa Serikali kupitia TANESCO imefanya kuwe na uhakika wa kufanya uwekezaji kwani kama hakuna umeme basi hakuna uwekezaji hasa wa viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Sailesh Pandit amesema kiwanda chao kinatumia umeme wa megawati saba ambapo kwa mwezi wanailipa TANESCO kati ya Sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kutokana na uzalishaji wake.
Amefafanua zamani kulikuwa na shida sana yaumeme lakini sana miaka miwili mitatu iliyopita maana umeme ulikuwa unatakatika mara kwa mara lakini sasa hali ni tofauti na hivyo lazima tuwapongeze Serikali na TANESCO kwa juhudi zao za kuboresha umeme.
”Ni kweli huko nyuma kulikuwa na shida ya umeme na sote ni mashahidi lakini leo hii hatuna tatizo la umeme tena.Kama tulipaza sauti kulalamika na hivyo hivyo tupaze sauti zetu kupongeza,”amesema Pandit.
Kuhusu ushirikiano wa kikazi kutoka kwa wafanyakazi wa Tanesco na kiwanda chake, amesema wanashirikiana vema na muda wote linapotokea Tanesco hata ikiwa usiku wa manane hupatiwa ufumbuzi wa haraka na kwa muda mfupi.
“Kwakweli sina cha kusema au kibaya chochote, namna ninavyofanya kazi nao ni very friend manner, mimi ninaweza kumpigia simu Injinia hata saa nane usiku, sina umeme ata respond simu yako hapo hapo na kuchukua hatua wakati kipindi cha nyuma haikuwa hiovyo.
Kwa upande wake Meneja Utawala na Rasilimali Watu wa Kiwanda cha nguo cha Sunflag, Magesa Charles, amesema kwa sasa huduma za umeme zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo matatizo madogo ambayo hayathiri shughuli za uzalishaji kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha A to Z, Viral Shah, amefafanua hakuna tatizo la kukatika kwa kama huko nyuma ila kuna wakati umeme unapungua nguvu.
“Kwa ujumla kumekuwa na maendeleo mazuri ya hali ya umeme ukilinganisha na kipindi cha nyuma, mwito wetu ni kufanyia kazi mapungufu hayo.Hapa kwetu tunatumia megawati 9 hadi 10 kwa mwezi na tunalipa bili zetu Tanesco Sh.bilioni 1.1 kwa kila mwezi na hapa tuna viwanda tisa,” amesema Shah.
Akizungumzia hali hiyo, Meneja Mwandamizi wa Miradi wa Tanesco, Mhandisi Emmanuel Munirabona, ameeleza kama shirika watafuatilia kwa kina kujua hasa nini chanzo cha tatizo hilo la kupungua kwa umeme katika kiwanda hicho.
“Tumefanya maboresho makubwa ya mitambo yetu ikiwa ni pamoja na kupanua vituo sita vya kupoza umeme jijini Arusha, ambavyo vimewezesha wateja wakubwa kufunguwa laini zinazojitegemea ili kuondoa uwezekano wa kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za uendeshaji.
“ TANESCO tumeamua kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa changamoto zote kama zipo , lengo letu ni kuhakikisha Tanzania ya viwanda inatekelezwa kwa vitendo na hii itatokana na uwepo wa umeme wa uhakika.
“Ndio maana tumeendelea kuboresha huduma zetu na lengo lake ni kuona hatuna matatizo ya umeme na tayari tumefanikiwa , hivyo tuendelee kutoa rai wawekezaji waje tu nchini kwetu kuwekeza kwani tunao umeme wa kutosha,”amesema.
Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Sun Flag kilichopo mkoani Arusha akitoa ufafanuzi kuhusu bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo
Mfanyakazi wa kiwanda cha TANELEC ambacho kinatengeneza trasfoma akiendelea na majukumu yake katika kiwanda hicho kilichopo Themi mkoani Arusha
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TANELEC wakiendelea na kazi ya kusuka transfoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha A to Z Viral Shah akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea kiwandani hapo kuona shughuli za uzalishaji
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z mkoani Arusha akiendelea na kazi kiwandani hapo
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z wakiendelea na majukumu yao wakati wa hariri wa vyombo vya habari nchini pamoja na maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) walipofanya ziara kiwandani hapo kuona shughuli za uzalishaji pamoja na hali ya upatikaji umeme kwa sasa
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC mkoani Arusha Zahir Saleh akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari(hawapo pichani) baada ya kutembelea kiwanda hicho ambacho kinatengeneza matransfoma ya umeme nchini
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh akiwaongoza wahariri na maofisa wa TANESCO kuelekea ndani ya kiwanda hicho ambacho kinatengeneza matransfoma ya umeme.Kiwanda hicho ni moja ya wateja wakubwa wa utumiaji umeme mkoani Arusha
Hivyo makala HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA
yaani makala yote HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/hatuna-tena-tatizo-la-umeme-katika.html
0 Response to "HATUNA TENA TATIZO LA UMEME KATIKA UZALISHAJI WETU,TUNAIPONGEZA TANESCO-WATEJA MKOANI ARUSHA"
Post a Comment