Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.

Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.
kiungo : Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.

soma pia


Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Mkoani Kagera, imehitimishwa Januari 02, 2019 kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.

Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine, Dkt. Bashiru amehitimisha kwa kuwataka wajumbe wa Kikao hicho kusitisha mchakato na mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya CCM, baina ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jasson Rweikiza pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba, Ndg. Murshidi Ngeze kuacha Mara moja kwani hauna tija wala faida ndani ya Chama, zaidi ni kuzorotesha Maendeleo.

Akirejea mgogoro huo kabla ya kusuluhisha, amenukuliwa akisema kuwa kumekuwepo na hali isiyokuwa ya kawaida kati ya Madiwani wanoumuunga mkono Mbunge na wale wanaomuunga mkono Mwenyekiti kuhusu wapi ijengwe Hospitali ya Wilaya ya Bukoba. 

Katibu Bashiru amethibitishia Kikao juu ya Kuomba radhi na Kukiri mbele ya Kamati ya Siasa kwa Mwenyekiti kuwa aliyumba kimaamuzi licha ya suluhisho kupatikana kuwa Hospitali ijengwe eneo la Kanazi kulingana na hoja za kitaalamu na Ukubwa wa eneo husika.

Kufuatia maelezo hayo Viongozi hao wawili Mbunge na Mwenyekiti wakapata nafasi ya kujieleza na kisha kumaliza tofauti zao za kisiasa huku Katibu Mkuu akimuomba Ndg. Rweikiza (MB) kurudisha malalamiko yake ndani ya Chama na sio Mhakamani kwa kile anacholalamika kuwa Ndg. Ngeze (Diwani Kata Rukoma) alimdhalilisha kwa kumtuhumu kuwa Mbunge Rweikiza alitoa Rushwa katika mchakato wa Uchaguzi. 

Tayari Mh. Rweikiza amekubali kurejea kwenye Vikao vya suluhisho na maadili ya Chama kulalamika upya, ingawa Dkt. Bashiru kaelekeza Viongozi hao kwenda kutoa ufafanuzi mzuri eneo la Ikimba ambalo baadhi ya watu walipotosha kuwa wametengwa kufuatia Hospitali kutojengwa eneo lao.

Aidha Dkt. Bashiru amepata nafasi ya kuwakaribisha rasmi madiwani waliorudi kutoka Vyama pinzani, huku kivutio kikubwa akiwa ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Kapteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Ndg. Kateme ambae baada ya kushindwa katika kinyanganyiro cha Uchaguzi katika Kara ya Kaibanja, alitimkia CUF na sasa ameamua kurejea kutokana na kuridhishwa na muundo wa Serikali iliyopo madarakani, na Utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza  wakati akihitimisha ziara yale leo Bukoba mkoani Kagera kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Baadhi ya Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa  katika Kikao chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.



Hivyo makala Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.

yaani makala yote Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dkt-bashiru-ahitimisha-ziara-yake.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM."

Post a Comment