title : DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU.
kiungo : DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU.
DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva akionesha DVD ya nyimbo ya wato yatima katika kitu cha Amani Foundatio cha Kigamboni Jijini Dar es salaam alipokwa akiizindua na kuweka jiwe la msingi na kuendesha harambee ya ujenzi wa kituo hicho (Picha na John Luhende).
Mwamba wa habari
Wito umetolewa kwa wazazi nalezi kutimiza wajibu wao kwa kuwaleo watoto badala ya kuwaacha bila uangalizi jambo ambalo limesababisha kuwa na watoto wasio na makazi maalumu.
Wito huo umetolewa na na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Felix Lyaniva wakati alikizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika harambee ya kuchangia ujenzi na uwekaji jiwe lamsingi ujenzi wa Kituo cha Amani cha kulelea watoto yatima kilichopo kibugumo Kigamboni Jijini Dar es salaam, na kuogeza kuwa kutekeza watoto ni dhambi kwa Mungu .
‘’Mtu ambaye anaacha familia yake na kuitelekeza na kuiacha ikihangaika huyo hata pata thawabu kwa Mungu ,kufanya hayo ni kukwepa wajibu ,napia wenye vituo hivi vya yatima naomba visiwe kwa faida ya mtu mmoja bali vifaidishe watoto na jamii”alisema
Jambo hili la kutelekeza watoto na kuwaacha mitaani linafanywa na baadhi ya wana jamii limekemewa pia na Katibu tawala Wilaya ya Kigambo Rahel Mhando ambapo ameitaka jamii kujiukiza na kuchukua hatua najukumu kwa watoto hao.
“Kwanini tunasema wanaoishi katika mazingira magumu wakati wana koo na familia zao walikotoka?jamii kwa namna moja amanyingine lazima itoe ushirikiano kuhakikisha hawa watoto wanapata huduma tena sisi ni waumini wazuri kilasiku kanisani msikitini lakini huyo mtoto mmoja wa ndugu yako amekushindaje?Alihoji
Kwaupande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Zubeida Makame , amwataka wanandoa kuishi kwa maelewano ili kuepuka mafarakano ya kifamilia ambayo yamesababisha watoto kuishia mitaani, na kusema kuwa yeye anatoa huduma kwa watoto hao na kwamba hajipatii faida .
‘’Malipo ya kazi hii ni kwa mwenyezi Mungu peke yake maana hii siyo biashara,malezi haya ni wito naombatu familia ziwe na uvumilivu ili walee wato wao walinde sana ndoa zao ili waishi vizuri na watoto wao wasifarakane ”alisema
Kituo cha Amani kina watoto zaid ya 50 , Majengo ya kituo hicho ili yaweze kukamilika jumla ya shigi milioni miamoja sabini na tano lakisaba na sabini elfu,lakini pamoja nakuendeshwa harambee hiyo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kumalizia ujenzi huo.
Hivyo makala DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU.
yaani makala yote DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dc-lyaniva-walezi-wazazi-msikwepe.html
0 Response to "DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU."
Post a Comment