title : BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY
kiungo : BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY
BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa tayari wameshamalizana na golikipa wao Beno Kakolanya ingawa wamepokea barua ya kuvunja mkataba.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo Samwel Lukumay amesema kwamba mlinda mlango Beno Kakolanya haidai klabu hiyo katika kipindi hiki baada ya kumaliziwa stahiki zake ambazo amekuwa akizidai.
Lukumay amesema ingawa wameweza kumaliza kumlipa stahiki zake zote, uongozi kwa siku ya jana umepokea barua kutoka kwa mwanasheria wa Beno wakihitaji kuvunja mkataba wake jambo ambalo amedai uongozi utakaa na kulijadili kwa undani kwani mchezaji alishalipwa stahiki zake kabla ya madai hayo ya kuvunja mkataba.
Amesema kwamba kimsingi hadi kufikia sasa mchezaji ni wa Yanga hivyo kama dhamira yake ni kuvunja mkataba basi ni vizur taratibu zikafuatwa.
Aidha amesema kwamba swala la yeye na kocha mkuu wa klabu Mwinyi Zahera ni jambo ambalo mchezaji alipaswa kuwasiliana na uongozi au kocha mwenyewe ili kulipatia ufumbuzi jambo ambalo hakulifanya.
Kwa mujibu wa Lukumay amesema kwamba katika usajili wa msimu uliopita Beno amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo bado angali na mkataba wa muda mrefu kusalia ndani ya klabu hiyo.
Hivyo makala BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY
yaani makala yote BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/beno-kakolonya-ameandika-barua-ya.html
0 Response to "BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY"
Post a Comment