title : BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA
kiungo : BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA
BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA
NA Yeremias Ngerangera…Namtumbo.
Mohamedi Mbawala (kasorobo)mkazi wa kijiji cha Mgombasi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma amemwokoa mtoto wake Mashaka mbawala (17)aliyeshikwa na mamba katika mto luegu.
Mashaka Mbawala alishikwa na mamba katika mto luegu wakati wa mchana akiwa na kaka yake Juma Mbawala (21)pamoja na kijana Awadi simba (18) wakioga katika mto huo.
Kwa mujibu wa Juma Mbawala ambaye ni kaka ya mashaka alisema walikuwa shambani pamoja na baba yao wakilima shamba na ilipofika majira ya saa nane mchana walimwomba baba yao ruhusa kwenda kuoga kupunguza joto na jasho mwilini kutokana na jua kali lililokuwa linaendelea wakiwa shambani hapo.
Baba yao Mohamedi aliwaruhusu wote watatu waende wakapunguze jasho na joto mwilini na kisha warudi shambani kuendelea na kulima kwa kuwa shamba lao hulima mpaka kwenye ukingo wa mto huo.
Watoto hao kwa pamoja walienda kwenye mto huo na kuanza kutoa jasho na mara mmoja kati yao akaanza kupiga kelele za kuhitaji msaada na wenzake baada ya kumwona mamba wakaanza nao kupiga kelele na ndipo baba yao alikuja haraka na panga na alipofika pale alimwona mwanae amechukuliwa na mamba na ndipo alipojitupa kwenye maji na kumfuata mtoto wake na kuibua ugomvi mkali kati yake na mamba.
Mohamedi Mbawala alidai aliridhika nayeye kupoteza maisha kuliko kumwacha mtoto wake aende huku yeye akimwona alimkata panga mamba mkiani lakini mamba huyo hakumwachia mwanae badala yake aliacha kumshika kwenye paja la mguu wa kulia akamshika kwenye goti na alipompiga panga la pili mamba huyo aliachia kwenye goti na kushika mguu maeneo ya vidole na alipompiga panga la tatu mgongoni alikubali kumwachia mwanae huku akiendelea kupambana nae eneo la mto huo likitapakaa damu tupu.
Baada ya mamba huyo kumwachia mwanae alimtoa nje ya mto na kumlaza kwenye mchanga akiwa amezimia kutokana na kunywa maji mengi alipigwa mchanga tomboni ili kuyaondoa maji na baadae mtoto huyo aliweza kupata ufahamu na ndipo walipomkimbiza Zahanati ya Mgombasi kwa Matibabu ya awali.
Mtendaji wa kata ya Mgombasi bwana Abeid kilosa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo amekimbizwa hospitali ya peramiho kutibiwa majeraha aliyopewa na mamba sehemu ya paja la mguu wa kulia ,kwenye goti na sehemu ya vidole katika mguu huo.
Afisa ardhi na maliasili bwana Saimon Sambalu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwahatarisha wananchi na vijiji vilivyopo kandokando na mto luegu kujihadhari kutumia maji ya mto huo kutokana na kutapakaa mamba katika mto huo.
Aidha aliwataka wazazi katika maeneo yanayopita mto huo kutowataka watoto wao kuoga ,kuchota maji katika mto huo wakiwa peke yao kwani kwa sasa mamba katika mto huo wameongezeka hasa nyakati hizi za masika ambapo maji yanakuwa mengi katika mto huo na mamba kusambaa katika maeneo mengi wakisaka chakula alisema Sambalu.
Kijiji cha mgombasi ni miongoni mwa vijiji vya Luegu,Mtonya na Libango wilayani Namtumbo vilivyogubikwa na matukio ya mara kwa mara ya watu kuliwa na mamba hasa nyakati za masika .
Hivyo makala BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA
yaani makala yote BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/baba-amwokoa-mwanae-kuliwa-na-mamba.html
0 Response to "BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA"
Post a Comment