AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE.

AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE.
kiungo : AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE.

soma pia


AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo kuitisha haraka Mkutano kwa Wadau wote wanaohusika na Mradi wa Maji Chalinze Jumanne ya Januari 29, mkutano utakaojadili changamoto za upatikanaji Maji katika Halmashauri hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada yakutembelea Mradi huo katika eneo la Chalinze, Mhe. Aweso amesema mpaka sasa mradi huo umefika asilimia 78 na Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kuhakikisha Wananchi wa Chalinze wanapata Maji yakutosha. 

Katika ziara yake hiyo, Mhe. Aweso amesema ameona changamoto katika uendeshaji wa mradi huo ikiwemo vituo vya Maji zaidi ya 200 lakini 86 ndio vinafanya kazi ya utoaji huduma ya Maji pamoja na changamoto ya uendeshaji ikiwa sambamba nakuwapa Watoto wadogo kusimamia vituo hiyo. 

Mhe. Aweso amewata Watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanatafuta Wakandarasi wenye weledi na kazi zao ili kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa ipasavyo bila kusuasua licha ya mradi huo kufika asilimia 78. 

"Mkandarasi anayesimamia mradi huu ni changomoto, hatuwezi kumuachia mpaka amalize mradi huu, tayari amechukua fedha zaidi ya asilimia 62 kwenye Bilioni 95", amesema Aweso

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze - DAWASA, Mhandisi Modesta Mushi amesema kuwa mradi huo umefika jumla ya asilimia 78 pamoja na ujenzi wa Miundombinu eneo la mtambo, ujenzi wa matenki kufikisha Maji maeneo tofauti na ujenzi wa vitekeo Maji (Viosk) jumla ya 351 maeneo mbalimbali katika eneo la mradi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa ameshukuru kuona ziara ya Naibu Waziri wilayani humo, amesema wataendelea kusimamia kuhakikisha Mkandarasi wa Mradi wa Maji, Chalinze anamaliza mradi huo kwa wakati licha kuahidi kumaliza Desemba 31, 2018, amesema wanahitaji kuona usimamizi mzuri katika Vitekeo Maji vilivyopo ili kutoa fursa kwa Wananchi wa Chalinze kupata huduma hiyo ya Maji Safi na Salama. 

Utekelezaji wa Mradi huo wa Chalinze, awamu ya tatu unatekelezwa na Mkandarasi Overseas Infrastructure Alliance (India) Private Limited pamoja na Kampuni ya Platiba kwa gharama ya Dollars za Kimarekani Milioni 41.1 ambao ni Mkopo wa gharama nafuu kutoka Serikali ya India.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akisaidia uchimbaji moja ya Mfereji utakaotumika kutandika mabomba katika eneo la mradi wa Maji, Chalinze.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja na Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze, Mhandisi Modesta Mushi katika eneo la mradi huo. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) (aliyevaa Kofia) akishuka chini pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa (aliyevaa Koti) baada yakukagua moja ya Tenki lililopo kwenye Mradi wa Maji, Chalinze mkoani Pwani. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Moja ya Tenki lililopo kwenye utekelezaji wa mradi wa Maji, Chalinze.


Hivyo makala AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE.

yaani makala yote AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/awezo-aitisha-mkutano-kujadili.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AWEZO AITISHA MKUTANO KUJADILI CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI CHALINZE."

Post a Comment