title : ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi
kiungo : ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi
ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Jukwaa la Katiba (ADO) imesema kuwa sheria ya vyama siasa baadhi ya wabunge waache kumhusisha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na sheria kwani yeye ndio aliyepigania uhuru na kufanya nchi ina amani. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Habibu Mchange amesema kuwa wabunge watumie weledi katika kujadili sheria hiyo kwani serikali ndio iliyopeleka ili vyama vya siasa viendeshwe kwa demokrasia na sio kama ilivyo kwa sasa.
Mchange amesema vyama vinajiendesha kwa kuwa na watu wale wale lakini sheria hiyo baada ya kupita na kuwa mswada kutakuwa na ukomo wa viongozi. Amesema kuwa kama wadau wanawajibu wa kuzungumza hali inayoendelea bungeni kwa masilahi mapana ya Taifa. Aidha amesema kuwa sheria ya vyama vya siasa haimpi nguvu msajili wa vyama kama yeye bali kazi hiyo inafanywa na ofisi ya msajili nchi nzima.
Amesema kuwa vyama vya siasa vimekuwa vikipewa fedha lakini haijowi pamoja na watu wengine wakichangia lakini zinatumika bila kuingiliwa na mtu yoyote hali hii inawafanya wanachama kukosa haki ndani ya vyama vyao hasa vyama vya upinzani. "Tunataka watu wajadili vitu vyenye hoja kwa mstakabali wa Taifa na kuondoa masuala ambayo yalikuwa katika vyama siasa vya kufanya visihojiwe katika matumizi ya fedha na madaraka ya viongozi wa wakuu".amesema Mchange.
Mchange amesema kuwa ndani ya sheria hiyo imeondoa kuwepo kwa vikundi vya ulinzi katika vyama ambapo vikundi hivyo vimekuwa vikifanya visivyo kwa kuwadhuru wasio na hatia.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jukwaa la Katiba (ADO) Habibu Mchange akizungumza na waandishi habari juu ya wabunge kujadili sheria ya vyama siasa kwa kuangalia masilahi mapana ya Taifa.
Hivyo makala ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi
yaani makala yote ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ado-yataka-wabunge-kujadili-sheria-ya.html
0 Response to "ADO yataka wabunge kujadili sheria ya weledi"
Post a Comment