title : Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu
kiungo : Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu
Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu
Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali nchini kinyume na sheria za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.
“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya historia ya mabadiliko ya Pasi za Kusafiria kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo, Sajini wa Uhamiaji, Vedasto Rweikiza(kulia), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma Panja(kulia), baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu
yaani makala yote Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wananchi-waaswa-kuwafichua-wahamiaji.html
0 Response to "Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu"
Post a Comment