title : Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio
kiungo : Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio
Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio
Na Raya Hamad OR-KSUUUB
Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora imedhamiria kuifanyia mapitio na kuimarisha sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mikakati yake ambayo ni moja ya nyenzo muhimu katika usimamizi wa utoaji huduma nchini.
Naibu Katibu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndugu Seif Shaaban Mwinyi anaeshughulikia masuala ya utumishi ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mwelekeo wa sera ya usimamizi wa Utumishi wa Umma na utekelezaji wake katika kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar
Ndugu Seif amesema Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawagusa wananchi wote wa Zanzibar hivyo ikiwekewa mkakati sahihi mafanikio yake yataweka misingi imara ya usimamizi wa huduma utowaji huduma na upatikanaji wa huduma bora za umma kwa kadiri siku zinavyokwenda .
Aidha amesema Sera tokea ilipotungwa mwaka 2010 yapo mambo mengi yaliyofanyiwa kazi katika utekelezaji na mafanikio makubwa yalipatikana ikiwemo Uundwaji wa Taasisi na vyombo mbalimbali vya usimamizi wa udhibiti katika utumishi wa umma, utungaji wa sheria na miongozo kusimamia na kudhibiti utumishi wa umma, marekebisho katika mifumo ya malipo ya mishahara pamoja na mafao baada ya kustaafu
Mifumo ya upangaji na uendeshaji watumishi , Ujenzi wa Ofisi za Kisasa, matumizi ya mifumo ya ki elektronik katika shughuli za utumishi wa umma ikiwemo kufungwa kwa kuwekwa mifumo ya habari na mawasiliano wizarani , ugatuzi wa majukumu kwa mamlaka za serikali za mitaa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii
Hata hivyo pamoja na juhudi zilizochukuliwa katika utekelezaji wa Sera bado kumekuwepo na changamoto kadhaa katika upatikanaji wa huduma za umma hapa nchini yakiwemo ongezeko la idadi ya watu jambo ambalo hulazimisha ongezeko la mahitaji ya huduma za umma, ongezeko la shughuli za kiuchumi na kukua kwa uchumi, kukua kwa ushindani katika Nyanja mbali mbali za uzalishaji
Kukua kwa matumizi ya teknolojia, miundombinu mbalimbali katika mahitaji ya kijamii na kiuchumi ni miongoni mwa mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa mikakati maalumu ambayo italeta mabadiliko yatakayoiwezesha Serikali kukabiliana na changamoto hizo .
Kiongozi na mkurugenzi wa mradi wa kusaidia watendaji wasio wa kitaifa wa Zanzibar Fergan Ryan amesema malengo na matarajio ya kikao hicho ni kutafakari kwa pamoja juu ya mpango wa utekelezaji wa mpango wa kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar na kuelezea hali halisi ilivyo kwa sasa changamoto na hatimae kupokea maoni na michango itakayosaidia kuzingatiwa katika uandaaji wa program ya pili mabadiliko ya Utumishi wa Umma
Nae Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Daima Mohamed Mkalimoto amesema Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar umeweka msisitizo wa kupatikana kiwango cha juu cha utawala bora na kuondokana na umasikini pamoja na kutambua umuhimu wa nafasi ya usimamizi wa Utumishi wa Umma katika kuyafikia malengo ya maendeleo ya Zanzibar.
Bi Daima amesisitiza washiriki hao na kuwakumbusha kuwa wote ni watumishi wa Umma na wanajukumu la kufanya kazi kwa kufuata Sera inayowaongoza hivyo kufanyakazi kwa uhakika kutaleta mageuzi kwa vile Sera inatamka kuwa “Dhima ya Utumishi wa Umma Zanzibar ni kutoa huduma bora kwa ufanisi na tija kwa umma wa Zanzibar na kwa kiwango cha juu cha uadilifu na heshima”
Aidha amewakumbusha washiriki hao kuwa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni msimamizi lakini Idara na Taasisi zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanalo jukumu la kuwahudumia wananchi na wajibu wa kutekeleza kwa vitendo badala kufanya kazi kwa mazoea.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa ni muhimu kufanyiwa mapitio kwa sera zilizopita kabla ya kuanza na sera mpya, masuala ya Utumishi wa Umma lazima taasisi ziungane pamoja na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi pia sheria zifanyiwe mapitio ili ziweze kufanyiwa kazi
Pia wamesisitiza suala la kuwekwa kwa kumbukumbu sahihi za watendaji na watumishi wa umma kwani wakati wakustaafu hutokea changamoto nyingi ikiwemo kujitokeza utofauti ya tarehe ya kuzaliwa kwa mhusika mmoja ambae huonekana katika vitambulisho vya ZSSF, Cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva , kitambulisho cha Mzanzibari , kitambulisho cha Benki nk jambo ambalo linapelekea usumbufu kwa jamii na watendaji
Mada zilizojadiliwa ni pamoja masuala ya usimamizi na uwajibikaji , tathmini, uwekaji wa kumbukumbu viinuwa mgongo, pencheni, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa kumbukumbu na taarifa , serikali za mitaa
Mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha maafisa watumishi na maafisa mipango kutoka Taasisi tofauti za SMZ na baadhi ya watendaji tofauti umeandaliwa na Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora unafadhiliwa kwa pamoja kati ya EU na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana
Hivyo makala Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio
yaani makala yote Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/sera-ya-menejimenti-ya-utumishi-wa-umma.html
0 Response to "Sera ya menejimenti ya Utumishi wa Umma kufanyiwa mapitio"
Post a Comment