MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO

MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO
kiungo : MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO

soma pia


MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO


Na Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mafunzo yametolewa kwa Maafisa Ugani 30 kutoka katika kata mbali mbali za wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kujua kanuni bora za kilimo cha kahawa yatakayosaidia kufufua zao hilo na kuhamasisha kilimo cha zao hilo ili kukuza pato la mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Dafrosa Sanga ni Meneja Uendeshaji wa Shirika la Cafe Africa lililoendesha Mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kujikita katika zao la kahawa kwani ni moja kati ya mazao yaliyopewa kipaumbele na serikali ikiwemo Korosho,pamba na chai.Dafrosa amesema kuwa mafunzo hayo huendeshwa kwa vitendo kuanzia kwenye kutesha miche,kuvuna na mnyororo wa thamani ili Maafisa Ugani hao waweze kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha kahawa.

Kipi Warioba ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi amewataka Maafisa Ugani hao wasikae Maofisini bali waende kupeleka ujuzi na marifa waliyoyapata kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa kahawa kwani uchumi wa mkoa huo umekua ukitegemea zao hilo kwa miaka mingi.Warioba alisema kuwa soko la kahawa la dunia bado linafanya vizuri hususan kwa kahawa bora imekua ikipata bei nzuri ukilinganisha na kahawa isiyokua na ubora imekua ikipata bei ya chini.

Mwakilishi wa Mafisa Ugani hao Magnus Mwang`ata alisema kuwa wanatarajia kuandaa mpango kazi pamoja na kuwa na mashamba darasa kila kata ili kuweza kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo bora cha kahawa kitakachowasaidia kuinua pato la mkulima.

Magnus alisema kuwa Mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza mbinu mpya za kilimo cha kahawa kwani teknolojia hubadlika kadiri miaka inavyokwenda hivyo ushirikiano wa Cafe Africa na Jukwaa la Wadau wa Kahawa (ANSAF) utawajengea uwezo Maafisa hao kukuza zao la kahawa.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiotesha Kahawa katika shamba darasa katika kijiji cha Mwasi Kusini


Hivyo makala MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO

yaani makala yote MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/maafisa-ugani-wanolewa-kufufua-kahawa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO"

Post a Comment