CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA

CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA
kiungo : CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA

soma pia


CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA

Na Benny Mwaipaja. WFM, Dodoma
CHUO Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kimeanza ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Ngozi na Kuzalisha Bidhaa za Ngozi katika Kata ya Idifu, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kitakacho gharimu zaidi ya shilingi milioni 500 kitakapo kamilika. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya wakati wa sherehe za mahafali ya 32 ya Chuo hicho Kampasi ya Dodoma, ambapo wahitimu 2,596 wametunukiwa vyeti na shahada mbalimbali.

"Kupitia mradi wa Eco Act, unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya, Chuo kimetekeleza falsafa ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ya Ujenzi wa uchumi wa viwanda hiki ambacho kikikamilika kitakuwa na jumla ya wafanyakazi 70, kati ya hao 50 watakuwa wa kudumu na vibarua 20" alisisitiza Prof. Mayaya. Aidha, Prof Mayaya ameeleza kuwa Chuo hicho kinatekeleza mradi mwingine wa kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi kwa kuzijengea uwezo Halmashauri za wilaya ya  Longido, Ngorongoro na Monduli mkoani Arusha ambao umepunguza changamoto za ufugaji katika jamii za wafugaji kwa kujenga mabwawa matatu ya kunyweshea mifugo.

"Mradi huu ni wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi za kimataifa za mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNCDF LoCAL), mashirika yasiyo ya kiserikali ya Haki Kazi Catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), aliongeza Dkt. Mayaya. Kwa Upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bi. Mugabe Mtani, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ya wananchi umelenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano iliyojipambanua kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akihutubia wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo hicho, Dodoma.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho  yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo, Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 32 ya chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho, Dodoma.
 Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakiwa katika sherehe za  mahafali ya 32 ya chuo hicho  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Maendeleo Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu,  wakati wa Mahafali ya 32  yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.   
(Picha na Saidina Msangi-Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA

yaani makala yote CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/chuo-cha-mipango-kuanzisha-kiwanda-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CHUO CHA MIPANGO KUANZISHA KIWANDA CHA KUCHAKATA NGOZI MKOANI DODOMA"

Post a Comment