title : BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA
kiungo : BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA
BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA
Na John Nditi, Morogoro
NAIBU Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema , Serikali inatarajia kufanya usanifu wa barabara ya Morogoro- Dodoma yenye urefu wa kilometa zipatazo 259 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kupata michoro na gharama halisi ili kujengwa upya kwa viwango cha ubora na mahitaji ya sasa .
Naibu Waziri alisema hayo mjini Morogoro alipofanya ziara ya ukaguzi wa matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali kutoka Dodoma hadi Moropgoro yakiwemo ya Kibaigwa , Gairo na kuangalia shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara ya Morogoro- Dodoma .
Alisema , licha ya kuendelea kuihudumia barabara kuu hiyo , kwa sasa Serikali imekuja na mpango mwingine wa kufanya usanifu kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 ili kupata michoro ambayo itaelezea gharama halisi ya kujenga barabara mpya katika kiwango cha ubora na mahitaji ya sasa.
Naibu Waziri alisema, Serikali inatenga fedha nyingi kila mwaka fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu ikiwemo ya Morogoro- Dodoma ili ziweze kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo ambapo kwa baabara hiyo iliyojengwa miaka zaidi ya 30 iliyopita kwa hali yake ya sasa imechakaa na kuzeeka.
Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akipata maelezo ya Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia) alipokagua shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara kuu ya Morogoro- Dodoma hivi karibuni na ( anayemfuatia Naibu Waziri ) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Doroth Mtenga.
Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akisisitiza jambo wakati akikagua shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara kuu ya Morogoro- Dodoma hivi karibuni na ( wapili kushoto) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Doroth Mtenga.
Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akikagua shughuli za ujenzi wa mizani mpya ya kisasa eneo la Dakawa Magereza barabara kuu ya Morogoro- Dodoma hivi karibuni akiongozwa na Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia) akiambatana na Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS ) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Doroth Mtenga ( wapili kushoto) pamoja na Wakala wa Mradi kutoka Kampuni ya Group Six International Ltd , Mhandisi Abdallah Rashid.( Picha na John Nditi).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA
yaani makala yote BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/barabara-ya-moro-dom-kufanyiwa-usanifu.html
0 Response to "BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA"
Post a Comment