title : Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo.
kiungo : Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wenzake wakipatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar kutoka kwa Meneja wa Studio hiyo Abeid Mfaume Faki alipotembelea Studio hizo Raha leo mjini Zanzibar.
Mhariri Picha za Video katika Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar Mohamed Abdulrahman akionyesha kazi wanazozifanya katika Studio hio kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wa Wizara hiyo.
Mhariri Picha za Video katika Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar Mohamed Abdulrahman akionyesha kazi wanazozifanya katika Studio hio kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wa Wizara hiyo.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wenzake wakipatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar kutoka kwa Meneja wa Studio hiyo Abeid Mfaume Faki alipotembelea Studio hizo Raha leo mjini Zanzibar.
Vijana wakimsikiliza Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla alipofanya mkutano nao katika studio ya Wasanii Rahaleo
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Na.Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar.
Imeelezwa kuwa Vijana ni hazina ya Taifa hivyo iko haja ya kubadilika na kujitambua kwa kuweza kubuni miradi mbali mbali katika Shehia na Wilaya zao ili iweze kuwapatia maendeleo yao .
Hayo aliyasema Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni, Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla wakati wa kikao cha Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo na Viongozi wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kila Wilaya ya Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo. Alisema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu kwa kuandaa mradi mkubwa katika kila wilaya ili uwe chanzo katika kusaida miradi midogo midogo itakayoanzishwa ndani ya shehia na kuwaletea maendeleo.
Alisema nia na madhumuni ya Wizara ya Vijana ni kuwakomboa vijana kutoka sehemu moja kwenda nyengine kwa lengo la kuhakikisha wanajiimarisha katika kupata ajira na kujikwamua na umasikini .
Aidha alisema Wizara imetenga zaidi ya shilingi billion tatu kwa ajili ya miradi ya vijana katika wilaya zote za Unguja na Pemba ili kuhakikisha lengo la Serikali la kuwakomboa vijana katika kukuza maendeleo linafikiwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Amour Hamil Bakari alisema mfumo mzima wa Baraza la Vijana bado linaonyesha halijakaa vizuri hivyo ipo haja ya kutumia busara kuliimarisha liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuona viongozi wanashirikiana na wanachama wenzao na watendaji wengine kutekeleza miradi watakayoanzisha kwa kiushindani .
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir alisema Baraza la vijana lilikuwa linakabiliwa na changamoto nyingi lakini jambo muhimu kwa sasa ni Wizara kushirikiana pamoja na Vijana ili kuona malengo ya kuwepo Mabaraza hayo linafikiwa.
Aidha alisema Serikali inania njema ya kusaidia juhudi za Vijana zinaimarika na kuhakikisha wanapata maendeleo kupitia miradi mbali mbali inayoanzishwa kuanzia ngazi ya Shehia, Wilaya hadi Mkoa .
Hivyo makala Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo.
yaani makala yote Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-wa-vijana-utamaduni-sanaa-na.html
0 Response to "Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo."
Post a Comment