WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI

WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI
kiungo : WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI

soma pia


WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI

Na Baltazar Mashaka, Mwanza
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza linakusudia kujenga hospitali itakayowahudumia waumini wa dini hiyo na jamii. Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke alisema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na waumini wa dini hiyo baada ya kufanya usafi kwenye Msikiti wa Nyegezi Kijiweni katika Wilaya ya Nyamagana.

Alisema baadhi ya wananchi wamevamia na kujenga kwenye maeneo yanayomilikiwana taasisi hiyo ya dini likiwemo eneo la msikiti wa Nyegezi Kijiweni wanalotaka kujenga kituo cha afya na baadaye hospitali na hivyo wote waliovamia maeneo yake waondoke wenyewe. Sheikh Kabeke alifafanua kuwa wamebaini maeneo ya BAKWATA mkoani Mwanza likiwemo eneo la msikiti wa Nyegezi ambao ulichomwa moto na watu wasiojulikana, yamevamiwa na kuwataka walioingia na kufanya ujenzi wajitathmini na wachukue uamuzi sahihi kwa maslahi ya Waislamu na jamii ya Watanzania.

Alisema waliojenga kwenye ardhi ya maeneo ya baraza hilo la Waislamu ni vema wakaondoka wenyewe badala ya viongozi wa kiroho kuingia kwenye mgogoro na misuguano isiyo ya lazima na waumini wake ama jamii inayowazunguka.Kaimu sheikh huyo wa mkoa alisema; “ Katika utaratibu wa BAKWATA wa kukagua na kuhakiki mali zake wamebaini baadhi ya maeneo yao yamevamiwa na kujengwa nyumba za kudumu.Waliovamia waje tukae mezani kwa mazungumzo ili wapishe kwa hiari badala ya kuingia kwenye migogoro na marumbano.”
 Katibu wa BAKWATA Kata ya Nyegezi akifafanua jambo kwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke wakati wakikagua mipaka ya eneo la taasisi hiyo Nyegezi Kijiweni. 
 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakiwemo waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye Msikiti wa Nyegezi Kijiweni katika Wilaya ya Nyamagana. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa BAKWATA mkoani humu, Sina Mohamed Mwagalazi.
 Ustadhi Khatibu Imani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) kuhusu uvamizi wa ardhi ya BAKWATA ulipojengwa Msikiti wa Nyegezi Kijiweni. Picha zote na Baltazar Mashaka

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI

yaani makala yote WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waliovamia-ardhi-ya-bakwata-mwanza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WALIOVAMIA ARDHI YA BAKWATA MWANZA WATAKIWA KUONDOKA KWA HIARI"

Post a Comment