title : WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA
kiungo : WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA
WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA
Na Karama Kenyunko,Blogu ya jamii
WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.
Washtakiwa waliofikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wametajwa kuwa ni Naushad Mohamed, Alfred Mhina, ,Joseph Mrema, Justine Mosha, Anuary Shampoo Pius Nyeregeti,ambapo imedaiwa na mwendesha mashtaka mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kuwa, kati ya Agosti 30 na Sepemba 9 mwaka huu, washtakiwa walikula njama ya kuiba Mali iliyokuwa ikisafirishwa.
Imedaiwa katika shtaka la pili kuwa, Septemba 8 mwaka 2018 katika eneo la Geti namba tano la TPA lililopo wilayani Temeke, mshtakiwa Nyeregeti, alijitambulisha kama Nassoro Mohamed kwa Gaspa Swai ambaye ni Ofisa wa TRA huku akijua kuwa si kweli.
Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao waliiba kontena lenye nguo zenye thamani ya sh. 177,608,761 mali ya Nkonde Bright ambayo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka Zambia.Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kujihusisha katika muamala uliohusiana na wizi wa nguo hizo huku wakijua mali hiyo ni zao la kosa la utangulizi la mali isafirishwayo.
Mbele ya Hakimu, Maira Kasonde imedaiwa na Wakili wa Serikali Eric Shija kuwa Septemba 18, 2018 washtakiwa Anuary Shapoo, Pius Nyeregeti, Athanas Nsenye, Yusuph Mkuja, na Ismail Hajji walikula njama ya kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa.Katika shtaka la pili imedaiwa washtakiwa waliiba contena lililokuwa na magunia 520 ya mahindi yenye thamani ya sh. 31,698,411 Mali ya Brian Mwacha ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Dar kwenda Zambia.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa kubadilisha magunia hayo na na fedha kwa kuyauza huku wakijua kuwa kosa hilo ni zao la kosa la utangulizi la wizi wa mali isafirishwayo kwa dhumuni la kupotezea uhalisia wa mali.
WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.
Hivyo makala WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA
yaani makala yote WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wafanyakazi-tisa-tpa-wafikishwa.html
0 Response to "WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA"
Post a Comment