VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA
kiungo : VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

soma pia


VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema serikali imeshaanza uhakiki wa wakulima wanaodai malipo ya korosho ambapo jumla ya vyama vya msingi 35 vimeshahakikiwa na malipo yameanza kufanyika.

Hayo aliyasema jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu opereshe korosho inayoendelea katika mikoa inayolima korosho kuhakikisha wakulima wote wanauza korosho zao kwa serikali kwa bei ya Sh. 3,300.

"Tulitenga vyama 50 vya awamu ya kwanza na ndani ya siku mbili tumehakiki taarifa za wakulima kwenye vyama 35 kwa kuangalia majina yao, kiasi cha korosho walichoingiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kulipwa na taarifa za akaunti zao na hivi ninavyoongea tayari wameanza kulipwa kuanzia sasa kupitia akaunti zao binafsi," alisema Hasunga.

Alitaja halmashauri ambazo vyama vyao vimehakikiwa kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Newala (5) Wilaya ya Newala (5) Wilaya ya Masasi (5) Nanyumbu (2) Lindi (5) Tunduru Ruvuma (5).Kuhusu malipo ya kitaasisi ikiwemo ushuru wa halmashauri alisema inaanda mwongozo wa kuangalia namna ya kuwalipa na kwamba malipo yatafanyika baada ya korosho kubanguliwa na kuuzwa.

"Ili kulipa malipo ya makato yote lazima tujue tumeuza korosho kwa bei gani kisha kama ni asilimia zinakatwa kulinga na bei tuliyouzia," alisisitiza.Makato hayo ya kitaasisi huwa yanalipwa kwa Halmashauri ambayo huchukua asilimia tatu ya bei elekezi, wasafirishaji wa korosho, watunza maghala pamoja na vyama vikuu vya ushirika ambavyo hukata Sh. 53 katika kila kilo moja ya korosho kwaajili ya vifungashio.

Hasunga yupo mikoa ya kusini tangu siku moja tu baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ili kujionea zoezi la uingizaji korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hazitoki na kuuzwa baada ya serikali kuweka msimamo wa kununua korosho zote za wakulima nchini.

Alisema kwasababu serikali ndiyo mnunuzi wa korosho hivyo inalazimika kulipa tozo ambazo walikuwa wanalipa wanunuzi wengine."Kwa agizo la Rais fedha zote zitapelekwa kwa wakulima bila makato yoyote kwasababu tunaangalia wakulkma kwanza na wengine watalipwa baadae" alisema.
Waziri wa Kilimo , Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kutoa Malipo ya korosho kuanzia leo Novemba 17 mwaka 2018 kama ilivyoagizwa na Rais Dr.John Pombe Magufuli.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wametoka kuokota korosho katika Mashamba ya shule kwa ajili ya kukusanya ziende kuuzwa kwenye Maghala.


Hivyo makala VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

yaani makala yote VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/vyama-vya-msingi-35-vimehakikiwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA"

Post a Comment