TANZIA .

TANZIA . - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZIA ., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZIA .
kiungo : TANZIA .

soma pia


TANZIA .

UONGOZI wa Bodi na Menejimenti ya Baraza la Kilimo Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mwakilishi wake katika Wilaya ya Wangi’ng’ombe Mkoani Njombe Bw. John Wihallah aliyefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Basi alilokuwa amepanda la Rungwe Express lilokuwa likitokea Dar es saalm kuelekea Mkoani Mbeya kwa kugongana na Gari aina ya Coaster katika eneo la Iyovi Mkoani Morogoro.

Bw. John alikuwa akitokea Jijini Dar es Salaam alikokuwa akishiriki Warsha ya Kitaifa ya Wadau wa Kilimo iliyofanyika Nov 26/27 na baadae kushiriki Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo uliofanyika Nov 28. 

Taarifa za kifo chake zimepokelewa kwa maskkitiko makubwa hasa ikizingatiwa Bw John alikuwa kiunganishi muhimu kati ya wakulima na Baraza la Kilimo Wilayani Wang’ing’ombe Mkoani Njombe,

Uongozi wa Baraza la Kilimo Tanzania utamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika Sekta ya Kilimo lakini pia Baraza limeahidi kufanyia kazi mapendekezo na ushauri wote alioutoa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania ambapo lipata fursa ya kuchangia masuala mbalimbali.

Mwili wa Marehemu John Wihallah unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Wilaya ya Wang;ing;ombe Mkaoni Njombe Jumapili Dec 02 Mwaka huu.

Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

Imetolewa na Baraza la Kilimo Tanzania,
Dar es salaam.
Nov 30, 201 

Ndugu John Wihallah (enzi za uhai wake) akishiriki mkutano mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania Nov 28, Jijini Dar es Salaam, kabla ya kufikwa na mauti Nov 29 alipokuwa akirejea Mkoani Njombe.


Hivyo makala TANZIA .

yaani makala yote TANZIA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZIA . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tanzia_30.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZIA ."

Post a Comment