title : SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI
kiungo : SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI
SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI
SERIKALI ya Norway imefurahishwa na jitihada zilizofanywa na serikali nchini katika kusimamia fedha walizotoa mwaka 1995 kugharamia miradi ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vilivyopo hapa nchini.
Akizungumza leo baada ya kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili, Waziri wa Maendeleo nchini Norway Nicolai Astrup, alisema walitoa fedha hizo kwa serikali kutokana na uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo ikiwemo usimamizi mzuri uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Waziri huyo pia alisema kuwa serikali yake imeongeza mkataba wa kusaidia uwekaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijiji kutoka mwaka 2020-2021 baada ya kuridhika na usimamizi mzuri uliofanywa katika ukarabati wa vituo hivyo.
“Nipo hapa Pangani Falls, Norway na Tanzania wanahusiano muda mrefu, nimekuja kufuatilia matokeo ya msaada tuliotoa mwaka 1995, kwa vituo vya kuzalisha umeme ‘Hydro Power Plants’,” alisema.

Baadaye akizungumza na wananchi wa mji wa Bagamoyo wilayani Korogwe Waziri huyo alisema kwamba nishati ya umeme ni muhimu katika maendeleo ya wananchi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kwamba serikali yao itanedelea kushirikiana na Tanzania kusaidia nishati hiyo.
Serikali ya Norway ilitoa kiasi fedha za Kimarekani dola milioni 126 awamu ya kwanza na kisha awamu ya pili ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vya New pangani Falls, Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Mtera ukarabati uliomalizika Aprili mwaka huu walitoa jumla ya shilingi bilioni 21.
NAIBU Waziri wa Nishati wa tatu kutoks kushoto akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara hiyo kukagua miradi wanayoifadhili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akiteta jambo na Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu.

Hivyo makala SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI
yaani makala yote SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-ya-norway-yaridhishwa-na.html
0 Response to "SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI"
Post a Comment