SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA
kiungo : SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

soma pia


SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe. 

Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya  uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Waziri Mkuu amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilembela wilayani Mbogwe akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita, Novemba 29, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Maabara ya Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazazi waliolazwa kwenye Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Frola Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Flora Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

yaani makala yote SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-kuwanufaisha-wachimbaji-wadogo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA"

Post a Comment