title : RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO
kiungo : RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO
RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji, Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye Stand Mpya ya Mabasi ya Msamvu kujifunza namna stand hiyo imefanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri.
RC Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa stand Mpya ya kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi Billion 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa Mara nne ya Stand ya Msamvu ambapo itakuwa na uwezo wa kupokea Mabasi 500 kwa wakati mmoja.
Aidha RC Makonda amesema Stand mpya ya Mbezi Luis itakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel,Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo,kituo cha polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.
Pamoja na hayo RC Makonda ameonyesha kufurajishwa na namna stand ya Msavu ilivyoweza kuweka utaratibu mzuri kiasi cha kuongeza mapato kutoka shilingi 350,000 hadi kufikia Shilingi Million 4.5 kwa Siku.
Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na wamesema watafika Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani Na nje ya nchi.
Hivyo makala RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO
yaani makala yote RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/rc-makonda-atembelea-stand-ya-mabasi.html
0 Response to "RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO"
Post a Comment