NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI
kiungo : NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

soma pia


NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye. 
Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye
Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 
Nditiye amesema kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 2.448 na kazi hiyo ilisimama kwa kipindi cha mwaka mzima mwaka 2017 na kuanza tena ambapo hadi sasa haijakamilika na imechukua kipindi cha miaka mitatu tofauti na mkataba wa awali ambapo ilitakiwa ijengwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Serikali hatuwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tunawatesa wananchi kwa kukosa huduma na kutumia vibaya fedha za Serikali,” amesema Nditiye
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita (hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua  wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi. Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

yaani makala yote NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/nditiye-takukuru-futuatilieni-ujenzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI"

Post a Comment