title : Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha
kiungo : Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha
Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WATANZANIA wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi wametakiwa kuendelea kutumia pasipo kuacha, ili waweze kuishi maisha yenye afya iliyoimarika hivyo kuendelea kulitumikia taifa. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati akifungua kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Alisema kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ambao walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU, asilimia 87.7 ndio wamefubaza VVU ambapo wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84. “Napenda kuhamasisha watanzania wote wanaotumia dawa za kufubaza VVU waendelee kuzitumia pasipo kuchoka na kwa kufanya hivyo wataweza kuishi maisha yenye afya iliyoimarika na furaha na hivyo kuendelea kulitumia taifa vyema” alisema Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Pima VVU, Jitambue Ishi ambayo inaonesha ushahidi kutokana na matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 hapa nchini.
Alisema utafiti huo unaonesha kuwa kama nchi bado hatujafanya vizuri katika kutimiza malengo 90 ya kwanza ya kimataifa yaani asilimia 90 ya WAVIU nchini wawe wamepima na kujua hali zao ifikapo mwaka 2020.
Mavunde alisema matokeo yameonesha ni asilimia 52 tu ya WAVIU nchini wanajua hali zao. “Hii ina maana kwenye eneo la kupima kuna vikwazo vingi vinavyowafanya watu hasa wanaume kutojua afya zao, pengine nchi bado hatujapata ufumbuzi bado kwani kutokana na matokeo ya utafiti huo ni asilimia 45 tu ya WAVIU wanaume wanajua hali zao” alisema
Alisema katika kutekeleza tisini ya pili yaani asilimia 90 ya WAVIU wajuao hali zao wawe wameanza dawa za ARV ifikapo mwaka 2020 kama nchi, imepiga hatua japo kwa kusuasua kidogo kwa upande wa wanaume. Alisema utafiti wa mwaka 2016/2017 umeonesha kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 ambao wanajua hali zao za maambukizi asilimia 90.9 walianzishiwa dawa za kufubaza VVU, wanawake wakiwa asilimia 92.9 na wanaume ni asilimia 86.1. Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, inaahidi kutoa ushirikiano. Alisema malengo hayo ni pamoja na kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2023 kama ilivyobainishwa kwenye mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI nchini na hatimaye kufikia malengo ya sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za UNAIDS wakati wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Wadau mbalimbali wanaoshiriki kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kisayansi la uwasilishaji wa matokeo ya tafiti za UKIMWI nchini kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2018 linalofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha
yaani makala yote Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/naibu-waziri-aomba-wanaotumia-arvs.html
0 Response to "Naibu Waziri aomba wanaotumia ARVs kutoacha"
Post a Comment