title : Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya
kiungo : Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya
Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya
Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Mradi wa Tuimarishe Afya(HPSSP) umeishauri jamii kujiunga katika Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya (CHF) ili kuweza kupata matibabu ya uhakika pale inapokumbwa na magonjwa na pamoja na kujipunguzia gharama za matibabu.
Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Afisa wa Mradi huo kutoka mjini Dodoma, Happiness Ning’o katika kilele cha Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Afya uliofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Amesema asilimia kubwa ya watanzania hawajiunga katika mifuko ya bima ya afya na kubainisha kuwa changamoto hiyo huchangiwa kukosekana kwa elimu ya kutosha huku akiitahadharisha kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo.
“Nawashauri wananchi kujiunga CHF unasaidia kipindi cha wakati mtu anapokumbwa na magonjwa hupata matibabu sahihi,” amesema.
Amebainisha kuwa mradi huo umeleta mapinduzi makubwa katika mikoa iliyofanyiwa majaribio na kusisitiza wananchi wengi wamejiunga na mfuko huo.
Amefafanua kuwa HPSS imefanikiwa kuzishauri halmashauri zilizofanyiwa majaribio kutumia mfumo wa kutumia mzabuni teule pale panapohitajika uharaka wa dawa.
Kwa upande wake, Mshauri wa Masuala ya Fedha wa mradi huo, Rwezaula Elizeus amesema HPSS ni mradi wa Serikali unaofadhaliwa na Serikali ya Uswisi na kwamba unasaidiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuona namna gani mifumo ya fedha inaimarishwa kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya
Ameyataja malengo ya HPSS ni kusimamia mfumo wa upatikanaji na usimamizi wa dawa na vifaa, upatikanaji wa fedha kwa ajili ya huduma za afya, usimamizi wa vifaa tiba katika Zahanati, vituo vya afya na hospitalini na elimu ya afya kwa jamii.
Aidha, amesema majaribio ya mfuko wa CHF yameafanyika katika mikoa sita ikiwemo ya Dodoma, Morogoro na Shinyanga ambapo asilimia zaidi ya asilimia 35 ya wananchi wa mikoa hiyo wamejiunga.
Katika hatua nyingine, amesema kiwango cha kujiunga kwa kaya ni Sh 30,000 kwa familia isiyozidi watu sita huku akikazia Serikali iko kwenye mchakato wa kuunganisha mifuko ya bima.
Rwezaula amesema tayari Serikali imeshatoa waraka ya utekelezaji wa wananchi kujiunga kwenye mfuko huo na kubainisha kila mkoa uko kwenye maandalizi.
Naye Daktari Ezekiel Mkuya amesema mradi huo umesaidia kuondoa mlolongo mrefu wa ununuzi wa dawa katika ngazi ya wilaya na halmashauri.
Hivyo makala Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya
yaani makala yote Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mradi-wa-tuimarishe-afya-waishauri.html
0 Response to "Mradi wa Tuimarishe Afya waishauri jamii kujiunga Mfuko wa Jamii wa Bima ya Afya"
Post a Comment