MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA
kiungo : MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

soma pia


MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

BENKI ya NMB imetoa semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa NMB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.

Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala wa NMB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi katika kumuhudumia mteja.

Alisema NMB ndio benki pekee yenye idadi kubwa ya mawakala zaidi ya 6,000 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 228 na mashine za ATM zaidi 800 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.

Akiwasilisha mada za mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia watanzania. Alisema malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na zawaadi wakala bora kwa mwaka 2018 Kandaa yaa Dar es Salaam kwenye semina kwa mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meza kuu kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wa jijini Dar es Salaam ikipiga picha ya pamoja na mawakala bora kwa mwaka 2018 wa Benki hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akizungumza na mawakala wa NMB kwenye semina kwa mawakala wa Benki hiyo wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Sehemu ya mawakala wa NMB waliohudhuria semina hiyo wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa.


Hivyo makala MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

yaani makala yote MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mawakala-wa-nmb-wapewa-semina-kuongeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAWAKALA WA NMB WAPEWA SEMINA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA"

Post a Comment