title : MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO
kiungo : MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO
MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali na kukubali kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ya kupinga kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kutupilia mbali hoja za pingamizi la Serikali ambazo ziliiomba Mahakama iitupilie mbali rufaa hiyo bila hata kusikilizwa sababu zina mapungufu kisheria.
Mbowe na Matiko wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 23, 2018 kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo inayosilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, Kutokana na maombi ya upande wa mashtaka, kwa madai ya kuwa wamekiuka masharti ya dhamana kwa kutokufika mahakamani tarehe ambazo kesi yao ilipangwa kwa ajili ya usikiljzwaji wa awali (PH).
Rufaa hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana lakini upande wa Serikali uliwasilisha pingamizi la awali ikitoa sababu tatu za kutaka rufaa hiyo itupwe ikiwemo kuwa rufaa hiyo iko mahamakani isivyo halali kwani inakiuka vifungu vya sheria.
Akitoa uamuzi leo Novemba 30,2018 Jaji Sam Rumanyika
amekataa sababu ya pingamizi la Serikali kuwa rufaa hiyo iko mahakamani isivyo halali.
Jaji Rumanyika amesema kuwa rufaa hiyo iko mahakamani kihali kwani si lazima kutaja kifungu cha kisheria kinachoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.
Hata hivyo amekubaliana na hoja za Serikali za kupewa mwenendo wa kesi ya msingi wa shauri hilo uliochapishwa ambao unasomeka vizuri. Pia Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja kuwa sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya mwezi Machi na April.
Hata hivyo imeelezwa kuwa rufaa hiyo itasikilizwa saa nane mchana.
Hivyo makala MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO
yaani makala yote MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mahakama-kuu-yatupilia-mbali.html
0 Response to "MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA SERIKALI KWENYE KESI YA MBOWE ,SASA KUSIKILIZA RUFAA YAO"
Post a Comment