title : KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA
kiungo : KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA
KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amesema ndani ya miaka mitatu ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli wamefanikiwa kupandisha kiwango cha Elimu na kuwaondoa wanyonyaji wa wakulima wa korosho maarufu kwa jina la 'Kangomba' Pamoja na kuimarisha huduma za Afya katika mkoa huo.
Byakanwa Amesema hayo leo Mkoani Mtwara alipokuwa akitoa Mukhtasari wa Mafaniko ya Serikali ya awamu ya tano katika sekta mbalimbali kwenye mkoa wa Mtwara.
"katika sekta ya elimu kulikuwa na dhana ya kuwa wanafunzi awapendi shule lakini tangu nimefika nimeweza kuweka mipango ya kuhakikisha kuwa elimu inakuwa katika hali sawa kwa kutengeneza mpango kazi ambao umeweza kusaidia kuongeza ufaulu kutoka mkoa wa Mwisho kitaifa mpaka kuwa mkoa wa nane kitaifa" amesema Byakanwa.
RC Byakanwa amesema kila mwalimu Mkuu amepewa mpango kazi hivyo Mimi sijapiga ngoma marufuku wala shughuli za kitamaduni hivyo nimewataka walimu watimize wajibu wao na kuacha kuwasingizia wakazi wa mtwara kwani walipoamua kufundisha ufaulu umeongezeka.
Katika hatua nyingine Rc Byakanwa amesema wameamua kusimamia zao la Korosho katika miaka hii mitatu lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanamnufaisha zaidi mkulima wa korosho pamoja na kuwaondoa watu hao ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakipata fedha haramu kupitia michezo hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Miaka mitatu ya mkoa huo katika serikali ya awamu ya tano
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano wa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa Kuelezea Miaka mitatu ya Rais Magufuli.
Hivyo makala KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA
yaani makala yote KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/kuna-mafanikio-makubwa-mkoani-mtwara.html
0 Response to "KUNA MAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA"
Post a Comment