title : JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA
kiungo : JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA
JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KONGAMANO la kwanza la kitaaluma la Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki limefanyika leo kwa kuwakutanisha wataalamu na baadhi ya wanafunzi waliosoma katika chuo hicho.
Akifungua kongamano hilo Katibu mkuu wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amepongeza juhudi zinazofanya na taasisi hiyo katika kuboresha sekta ya afya na anafurahi kuona wanafunzi bora wanatoka katika chuo hicho ambacho aliwahi kufundisha wakifanya kazi ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikifanya vizuri na mchango wao katika sekta ya afya unaonekana na wao kama Wizara wapo bega kwa bega katika kuhakikisha wanaimarisha vyema sekta ya afya nchini.
Dkt. Mpoki amewataka wahitimu na wanafunzi kujiunga katika taasisi mbalimbali za afya na ameshauri kuwa kongomano hilo liwe endelevu katika kuimarisha na kufikia malengo waliyojiwekea ambayo yataonesha uimara na ubora wa taasisi hiyo.
Aidha amesema kuwa taasisi hiyo lazima ijijenge ili kuweza kuendelea kudahili wanafunzi wengi bora na hilo litafanikiwa kama wahitimu watafanya kazi zenye thamani za kutangaza taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika kongamano la kwanza la kitaaluma katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki ambapo amewapongeza kwa kutoa mchango katika sekta ya afya na kuwataka kuongeza idadi ya wadahiliwa katika chuo hicho.
Rais wa kongamano la kitaaluma chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hurbet Kairuki Dkt. Leonard Malasa akizungumza na hadhara wakati wa kongamano hilo ambapo amesema kuwa wanashirikishana ujuzi na kushirikiana ili kuweza kukuza hadhi na thamani ya chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu (taaluma) wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dkt. Moshi Ntabaye akizungumza wakati wa kongamano la kwanza la kitaaluma kufanyika chuoni hapo ambapo amesema kuwa wamejizatiti katika kuhakikisha wanashiriki vyema katika kuimarisha sekta ya afya nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikabidhi zawadi kwa Michael Kalimba mmoja ya kati wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2018, kulia ni makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa. Charles Mgone na kushoto ni Rais wa kongamano hilo Dkt. Leonard Malisa.(Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA
yaani makala yote JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/juhudi-za-hkmu-zapongezwa-washauriwa.html
0 Response to "JUHUDI ZA HKMU ZAPONGEZWA, WASHAURIWA KUONGEZA IDADI YA WADAHILIWA"
Post a Comment