title : GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI
kiungo : GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI
GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI
Mwambawahabari
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Methusela Gwajima, amemuomba Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Edward Lowasa, kufanyia kazi ushauri aliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Gwajima ambaye pia ni Mwanasheria kitaaluma, amesema Kitendo cha Lowasa, kuhudhuria na kuungana na serikali katika miradi ya maendeleo ni cha kuigwa na wapinzani wengine.
“Kitendo hicho kina onyesha kuwa Lowasa amekomaa kisiasa, ndiyo maana haoni tabu kuhudhuria katika shughuli za maendeleo tofauti na wapinzani wengine ambao wao kazi yao ni kuishambulia serikali mda wote kiasi kwamba hawaoni mazuri yoyote yanayofanywa na serikali”.
“Unajua kuna watu wao siku zote wanapenda kuona Tanzania inachafuka na haitawaliki, watu hawa hawajui ni kiasi gani Rais wetu Magufuli anafanya kazi Usiku na mchana kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo”.
Ninampongeza sana Mh. Lowasa kwani yeye ameamua kujipambanua wazi ya kuwa hapendi siasa za fujo, chuki binafsi, vurugu, uchochezi kwa sababu yeye hayo mambo sio sehemu ya maisha yake.
“Sasa kuna watu wamenuna na kukasirika baada ya kumuona Mh. Lowasa
anampongeza Mh. Rais Magufuli tena kwa bashasha tele, nawaambia hawa watu wenye mlengo wa siasa chafu, Watasubiri sana, kwani Mungu yupo pamoja na Rais Magufuli, ndio maana hasikilizi, hatishwi wala kubabaika na makelele yao, bali anapiga kazi tu na kuendelea kutekeleza ilani ya CCM kwa kasi kubwa katika sekta zote za miundombinu, Afya, Maji, Elimu, Ulinzi, Nishati n.k”.
Mwanzoni kuna watu walisema Hii ni Nguvu ya soda, lakini sasa sote tunaona na kushuhudia ya kuwa kila kukicha Mh. Rais wetu anaongeza kasi zaidi ya kuwatumikia watanzania kwa spidi ya Moto wa Gesi.
“Kwa mambo makubwa anayoyafanya Mh. Rais, tusitegemee yakuwa watu wote watampenda,” hivi ni nani asiyejua kuwa Mh. Rais Magufuli ameamua kutoa maisha yake kwa ajili ya nchi yake ?
“Hivi ni nani asiyejua kuwa linapokuja swala lenye maslahi ya nchi yetu Rais, Magufuli kamwe haogopi mtu yoyote ?
“Jamani! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hongera sana Mh. Rais Magufuli kwa uzalendo wako mkubwa ulionyesha katika nchi yetu,
“We will keep on supporting you”
“Ndio maana hata fitina zote zinazopangwa za kuichonganisha nchi yetu siku zote zinabainika haraka, na kila mbinu chafu inayopangwa gizani juu ya Rais wetu inafichuliwa mchana kweupe”
Ninamtia moyo Rais Magufuli azidi kusonga mbele kwani watanzania wengi wazalendo wako pamoja na yeye, acha hao wachache ,vibaraka waendelee kupoteza muda wao bure na kamwe hawatafanikiwa, Kwani watanzania walishawajua.
Itakumbukwa kwamba baada ya Chadema kuangukia pua katika chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zilizopita, Gwajima alimshauri Lowasa kuepuka kukaa karibu na washauri wabaya waliomzunguka kwani mda wake wa kufanya siasa za kwenye majukwaa umekwisha na alimshauri kustaafu siasa ili kulinda heshima yake.
Mwisho, Mh.Gwajima amewaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais Magufuli na amewataka wanasiasa kutanguliza uzalendo katika nchi yao huku wakijifunza Kutii sheria bila shuruti, Vinginevyo Watapata Tabu Sana.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Hivyo makala GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI
yaani makala yote GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/gwajima-ampongeza-lowasa-ampa-neno-zito.html
0 Response to "GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI"
Post a Comment