Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia
kiungo : Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

soma pia


Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Archiula mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho. Mhe. Naibu Waziri aliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo pamoja na kufanya mkutano na Uongozi wa chuo na Wakufunzi. 

Katika mkutano huo, uongozi wa chuo pamoja na Wakufunzi walitumia fursa hiyo kumwelezea Dkt. Ndumbaro changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwa ni pamoja na ufinyu wa majengo kulingana na mahitaji ya chuo na uchache na uchakavu wa miundombinu ya kufundishia.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri alitumia ziara hiyo kujua mikakati mbalimbali waliyojiwekea chuoni hapo ikiwa ni pamoja na dhamira ya kujenga majengo mapya ambayo ramani ya mchoro wa majengo hayo iliwasilishwa kwa Mhe. Naibu Waziri.

Kwa Upande wa Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuupongeza Uongozi pamoja na Wakufunzi wa chuo cha Diplomasia kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto wanazokumbana nazo. Aidha, alitoa rai kwa Uongozi wa Chuo pamoja na Wakufunzi wawe wabunifu zaidi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Archiula akimwelezea jambo Dkt. Ndumbaro huku Naibu Mkurugenzi wa Masomo Prof. Kitojo Wetengere akisikiliza kwa makini. 
Mkutano ukiendelea 
Dkt. Ndumbaro akionyeshwa na kuelezewa ramani yenye mchoro wa majengo ya kisasa yatakayo jengwa katika eneo la Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam .



Hivyo makala Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

yaani makala yote Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dkt-ndumbaro-atembelea-chuo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia"

Post a Comment