Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China
kiungo : Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

soma pia


Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Viongozi hao walijadili namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan wa kibiashara ikiwemo mchakato wa kampuni ya Equinor wa kuzalisha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kusafirisha nje ya nchi. 
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto akiongea wakati wa mkutano wake na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Magabilo Murobi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga na Afisa Dawati, Bi. Tunsume Mwangolombe
Balozi Zhui Yuxiao, Mwakilishi kutoka China anayesimamia masuala ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. Mwingine ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katikati akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura hayupo pichani. Wengine ni Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Magabilo Murobi na Afisa Dawati, Bi. Lillian Kimaro. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura katikati akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. Mhe. Naibu Waziri pamoja na mambo mengine ameleta ujumbe kuwa Venezuela inataka kufungua ofisi ya ubalozi nchini jambo ambalo Mhe. Mahiga amelikaribisha kwa mikono miwili na kueleza kuwa endapo Venezuela itafungua ubalozi itakuwa nchi ya nne kutoka Latin Amerika kuwa na ofisi ya Ubalozi Tanzania. 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto ukiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu anayesimamia Maendeleo na Ushirikiano kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, Bi. Trine Rask Thygesen. Katibu Mkuu alikuja kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya haki za binadamu na kuihakikishia Tanzania kuwa haijasitisha msaada wake kwa Tanzania.
Katibu Mkuu anayesimamia Maendeleo na Ushirikiano kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, Bi. Trine Rask Thygesen wa kwanza kulia akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahig.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

yaani makala yote Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dkt-mahiga-akutana-na-viongozi-kutoka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China"

Post a Comment