title : DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO
kiungo : DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO
DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo ameamua kufanya ziara katika Kata za Rwinga na Namtumbo kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.
Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.
Taarifa ya ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Mkuu wa idara ya maji alitoa majibu kwamba wanatoza 7000 flat rate kwasababu hakuna mita za maji katika baadhi ya maeneo.Hata hivyo Mkuu wa wilaya ameiagiza idara ya maji iwaandikie EWURA kuomba kupewa mita za maji haraka ili wananchi walipe kwa haki kutokana na maji wanayoyatumia kwani sio haki kuwalipisha Sh.7000 kwa kuchota maji mara nne tu kwa mwezi tena kwa uchache.
Pia wananchi walitoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya huyo kuwa katika kituo cha afya Namtumbo kuna wakati dawa hawapati na
wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa. Pia hakuna huduma za haraka kwani watendaji wa kituo cha afya wanachukua muda mrefu kuingiza taarifa kwenye komputa badala ya kuhudumia mgonjwa.
Hivyo Kizigo amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe kabla dawa hazijaisha kabisa awe ameshaagiza zingine ili ziwepo wakati wote. Lakini pia ahakikishe anaagiza dawa zinazotosha kata mbili (Rwinga na Namtumbo) kwani ni dhahiri kituo kinazidiwa na idadi ya wagonjwa kwani kinahudumia kata mbili badala ya moja.
Kuhusu matumizi ya kompyuta amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe mafunzo kwa vitendo yanatolewa na kufanyika ili kuongeza kasi ya watumishi kuhudumia watu kwa kutumia kompyuta kwani bado hawajazizoea katika kufanya kazi zao. Pia wakati huohuo kama kuna
mgonjwa amezidiwa waweke kipaumbele katika kumhudumia hata
kama hawajamaliza kuingiza taarifa kwenye kompyuta.
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akizungumza na Wakazi wa Kata za Rwinga na Namtumbo,alipofanya ziara yake kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.
Hivyo makala DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO
yaani makala yote DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dc-ajitosa-kuhamasisha-uhifadhi-wa.html


0 Response to "DC AJITOSA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA WILAYANI NAMTUMBO"
Post a Comment