title : Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali
kiungo : Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali
Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali
Mbunge wa Segerea (CCM )Bonah Kaluwa akiwa katika hafla fupi na Wanawake wa UWT Kata Kimanga Dar es Salaam leo (Kulia)Mwenyekiti wa UWT DKT.Tukay Picha na Heri Shaaban
NA HERI SHAABAN
Mwambawahabari
MBUNGE waJimbo la Segerea (CCM) Bonah Kaluwa amewataka Wanawake wa Jimbo hilo kuchangamkia mikopo ya Serikali isiyo na riba.
Kaluwa aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa akizungumza na Wanawake wa UWT Kata ya Kimanga na Kisukuru wakati alipopokea wanachama wapya 300 wa UWT katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Kimanga kwa kushirikiana na Kisukuru (A).
"Serikali umetenga imetenga fedha za mikopo isiyo na riba katika jimbo langu wamama,vijana changamkieni mikopo hiyo ili muweze kukuza mitaji yenu" alisema Kaluwa.
Kaluwa aliwataka Wanawake wa Jimbo la Segerea Manispaa ya Ilala kukopa pesa hizo na kuzitumia kwa malengo yaliokusudiwa sambamba na kupeleka marejesho ya mikopo ili wengine waweze kukopa.
Aidha kwa upande mwingine Kaluwa alisema yeye ndio Mbunge wa Jimbo la Segerea ndio atatatua changamoto za Wananchi kwa sasa yupo Jimboni kwa ajili ya kushughulikia kero zote.
Alisema anatarajia kuandaa mkutano Mkubwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wake hivyo wasikate tamaa,miradi yote itatekekezwa kwa fedha za Serikali .
Wakati huohuo Kaluwa alisema mikakati yake kila kata litafunguliwa GULIO ili waweze kupata fursa waweze kujishughulisha Wanawake na vijana katika ndani ya jimbo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Vijana wa kata hiyo ambao waliokuwa bado kukamilisha usajili wa vikundi kutumia fursa hiyo kusajili ili wote wachukue mikopo isiyo na riba ambayo inatolewa na Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli.
Dkt.Tukai aliwataka wanawake kujikwamua kiuchumi katika kujishughulisha na biashara na kukuza mitaji yao kuacha maisha tegemezi .
Pia aliwataka wanawake kuchangamkia fursa za biashara na kutangaza bidhaa zao katika masoko mbalimbali.
Naye Katibu wa UWT Kisukuru A Joyce Ngalunda alisema UWT Kisukuru ulianzishwa 1999 ikiwa na wanachama 62 mpaka 2018 walifikia wanachama 80.
Joyce alisema Novemba 28 mwaka huu imepokea wanachama wapya 300 ambao waligaiwa kadi za UWT na Mbunge Bonah Kaluwa katika hafla fupi ,Kisukuru A ina mashina 14 na mapya yanatarajia kuzinduliwa manne.
Jocye alisema dhumuni kuu kuakikisha Wanawake wote Wanapiga kura na kujikwamua kiuchumi ambapo wanawake wote wameshapewa elimu ya ujasiliamali pia wametuma maombi kwa Ofisa Mtendaji Kata kwa ajili ya kupatiwa eneo la biashara
Akielezea mikakati ya UWT Kisukuru A wamebuni kuwa na miradi ya pamoja ambao utasimamiwa na UWT tawi Mkaa wa mti ambao utagharamia shilingi milioni 1.5 Pia imeunganisha vikundi 25 vya Ujasiriamali kwa sasa wapo katika hatua za kutambulika kiserikali waweze kuchukua mikopo hiyo.
Hivyo makala Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali
yaani makala yote Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/bonah-awataka-wanawake-wachangamkie.html
0 Response to "Bonah awataka Wanawake wachangamkie mikopo ya Serikali"
Post a Comment