title : BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING
kiungo : BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
BALOZI wa China nchini Dk. Lu Youqing na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya kikao cha kazi ambapo wametumia kikao hicho pia kuzungumzia masuala yanayohusu uwekezaji hasa kwa kampuni za kutoka nchini China.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam ambapo Mwambe ametoa ufafanuzi pia kuhusu sheria ya kutoa vivutio vya uwekezaji hasa vinavyohusu msamaha wa kodi kwa wawekezaji huku akiendelea kutoa ufafanuzi zaidi kuwa kampuni za Kichina ziache kutumia taarifa za madalali na badala yake wafike TIC kupata taarifa mbalimbali za nchi kuhusu uwekezaji.
"Kituo hakipo hapa kukwamisha mwekezaji, tupo kwa ajili ya kusaidia kuanzisha uwekezaji wake nchini kwa kuwa tunatambua umuhimu wa uwekezaji huo kwa nchi,"amesema Mwambe.

Baada ya maelezo hayo Balozi ameridhishwa na amepongeza Serikali kwa kusimamia uwekezaji kwa uwazi na kufuata sheria na China inafurahia jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuboresha mazinga ya biashara na uwekezaji nchini."Mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa na ndiyo sababu kubwa ya makampuni mengi ya China kuendelea kuonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania,"amesema Balozi.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe kilichofanyika kwenye ofisi za Kituo hicho jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe (kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (kulia) walipokutana jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu Youqing (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe (wa pili kushoto).
Hivyo makala BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING
yaani makala yote BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/balozi-wa-china-nchini-tanzania.html
0 Response to "BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA DK.YOUQING"
Post a Comment